LADY JAYDEE AWACHARUKIA GLOBAL PUBLISHERS

LAdy JD

Lady Jaydee

Baada ya misukosuko kuikumba ndoa ya gwiji wa muziki wa Bongo Fleva, Lady Jaydee na mumewe mtangazaji, Gadner G. Habash, Gazeti moja la udaku ambalo huchapishwa na kusambazwa na kampuni ya Global Publishers iliandika habari iliyoonekana kumchefua  na kumvunjia heshima Anaconda.

”Jide, Dogodogo gumzo mjini” ilisomeka sehemu ya mbele ya gazeti hilo huku picha ya kijana huyo akionekana akiwa kwenye mkoko wa Jaydee aina ya Range Rover Evoque na picha nyingine ikiwaonyesha wakiwa katika pozi la kawaida kama wanavyoonekana hapo chini.

jide

Jide atiririka …Zamani ilikuwa haipo sehemu ya kujitetea, gazeti likishaandika ndio limeandika.  Lakini sasa ulimwengu umebadilika, sio muda wa watu wote kulishwa chakula kisichofaa.

Kwanza hicho kichwa cha habari kimenivunjia heshma sana Nafikiri lengo ni kuilazimisha jamii inayomuelewa JayDee tofauti imuone kuwa ni mtu asiefaa, sawa.

Dogo anaswa na mkoko? Huo mkoko mmemnasa nao wapi wakati hizo picha ni mimi nilizi post mwezi February Instagram????? Picha ambazo zilipigwa Nyumbani lounge tena kutumia simu ya Gardner.

Jide, dogodogo gumzo mjini 🙆🙆🙆🙆 Gumzo ni kitu kinachoongelewa sana na kilichoenea kila kona ,,,,,sasa hii habari ni gumzo wapi ambapo haisikiki, …… Mngeandika tumeamua kumuanzishia Jide gumzo hili, ndio ningewaelewa. Vitu vya kuzua.

Ni watu wengi tu wakija band wakipata nafasi wanaomba kupiga picha na mimi na wengine pia wanaomba kupiga picha na gari sababu wanaipenda.  Kama mtu yoyote anavyoweza kupiga picha na sanamu la kitu chochote anachokipenda.

Hivi je! Wimbo wa JayDee mgumba, JayDee tasa umechuja? Umeisha chati?? Nashangaa na najiuliza tu Inawezekana wimbo huo umechuja ndio maana mnatafuta wimbo mwingine utakao hit zaidi ya ule Ndio kinachopelekea kuandika story za namna hii 🙉🙉🙉🙉🙉🙉🙉🙉

Sio nyinyi mliokuja kuomba radhi kwa yote mliowahi kuniandika na kudai kuwa mmejirekebisha, miezi kadhaa tu iliopita? Sio boss wenu aliemfuata Gardner na kumwambia tumalize tofauti zetu?  Kama hizo tofauti zilikuwepo 😎😎😎 Inawezekana nyie ndio mna tofauti na mimi, sijawahi kuwa na tofauti na mtu hata nisiemfahamu. ..

Nashukuru Mungu nilikataa msamaha wenu ni kama nilihisi hamkumaanisha  Au sababu sijawahi kukubali show mlizotaka kufanya na mimi?
Je! Hiki ni kisasi? Sielewi  Mungu alienisimamia ataendelea  Hii sio vita ya kwanza wala ya mwisho  Dunia ni mapambano.

Kama nia ni kufanya niishi maisha ya uoga, kudhoofika na msongo wa mawazo mmefeli ,,,,, wengine mkijidai ni wacha Mungu huku mkiumiza nafsi za watoto wa binadamu wenzenu. No wonder mnaishi bila amani mbali na utajiri mlionao kwa kuogopa visasi.

Sikuzaliwa kukata tamaa  Pia wapo wanaopenda kuandikwa kwenye hayo magazeti yenu Wafanyieni favor ya kuwapa hiyo nafasi mi sifanyi muziki wa magazeti ya udaku  Mkiachana na mimi nitashukuru sana

Hata ndoa yangu ikivunjika haimaanishi mnitafutie story za kunichafua Ndoa ya Madiba ilivunjika sembuse yangu nina utofauti ipi na binadamu wengine?  Nyie ndoa zenu ziko perfect si ndio?  Hewala watakatifu nyie, mnaoficha yenu na kutangaza ya wenzenu.

Mwisho nawaomba watu mnaonielewa kutoamini tu habari yoyote ambayo haijatoka kwangu wala kwa muwakilishi wangu ambae ni “Webiro Wakazi Wasira”. Kama kuna chochote cha watu kujua nitakiongea mimi kwa mdomo wangu sio kuwekewa maneno mdomoni.

Kila siku ooooh tulimpigia simu hapatikani, namba yangu yenyewe kwanza hata mnaijua??? Mngekuwa mnaijua msingekuwa mnahangaika mnawapigia watu wangu wa karibu kunitafuta , na hao watu hawawezi kunisaliti ndio sababu mpaka miaka 70 mtaishia kusema tulimpigia simu JayDee hapatikani. Nyie muongee chochote mnachojiskia Ila sie hatuna haki kujitetea ??

Hili nalo litapita kama mengine  Na inshallah nitakuwa hapa hapa nimesimama nawaangalia

Picha moja wapo ni hiyo ambapo mtoto wa vitoto alikuja siku hiyo hiyo na akapiga picha na Gardner, mbele ya gari hiyo hiyo mnayodanganya watu kuwa mmemkuta nayo na mahala ni hapo hapo Nyumbani Lounge, ,,,,, na picha nyingine ni hizo nilizowahi kuzi post mimi mwenyewe mwezi february leo zinanihukumu endeleeni kudanganya jamii

Na hizo ni chat alizoniandikia huyo mtoto wa vitoto ambae ndio ilikuwa mara yangu ya kwanza kumuona na sijawahi kumuona tena. . Zaidi ya kuongea nae twitter ,,, sisemi kama mimi malaika lakini
Ukweli huwa hauchanganywi na uongo

Kwa hili mmenidhalilisha sana  Kama nia yenu jamii inione mwanamke nisiefaa na ninaependa dogodogo  Basi Mungu atawaonyesha ukuu wake”

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s