DWYANE WADE NA GABRIELLE UNION WAFUNGA NDOA

dwayne-wade-1024Hayawi hayawi sasa yamekuwa, Staa wa filamu kutoka Hollywood Marekani, Gabrielle Union amefunga pingu za maisha na mchumba wake wa muda mrefu mcheza kikapu wa  Miami Heat ‘Dwyane Wade’  hapo jana (Agosti30).

Ndoa ya mastaa hao ilifungwa mjini Miami na kuhudhuriwa na ndugu pamoja na marafiki wa karibu sambamba na burudani ya aina yake iliyotolewa na mwanamuziki John Legend.

Hii inakuwa ni ndoa ya pili kwa wote wawili, kwani hapo awali Wade alifunga ndoa na mchumba wake wa sekondari ‘Siohvaughn Funches’ mwaka 2002 na kufanikiwa kupata watoto wawili Zaire na Zion kabla ya kutemana mwaka 2007 halikadhalika na kwa Gabrielle ambaye aliolewa na mchezaji  wa NFL ‘Chris Howard’ mwaka 2001 na kuachana mwaka 2006.

Itakumbukwa mwezi March mwaka jana, Wade mwenye miaka 32 alimvisha pete ya uchumba ya almasi  Gab(42) katika sherehe ndogo iliyohudhuriwa na mastaa kama  vile Jamie foxx, Kevin Hart  na Kelly Rowland.

 

Wade na Gabrielle katika pozi

Wade na Gabrielle katika pozi

Gabrielle UnionWedding4

Gabrielle Union akiwa na mbunifu wa gauni lake la harusi Dennis Basso

GabrielleUnionWedding1

 

 

 

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s