MCHUCHU MPYA WA BIG SEAN AGOMA KUMWAGA MCHELE KWENYE KUKU WENGI

Big sean na Ariana Grande

Big sean na Ariana Grande


Kinda wa miondoko ya R&B kutoka majuu, Ariana Grande amegoma kabisa  kumwaga mchele kwenye kuku wengi juu ya kile kinachoendelea kati yake na Rapa Big Sean wakati alipofanyiwa mahojiano na mtangazaji maarufu Ryan kwenye Ryan Seacrest Radio Show.

Ariana mwenye umri wa miaka 21  alijikuta akimung’unya maneno baada ya kuulizwa kama yupo kwenye mahusiano ya kimapenzi na Big sean ambaye  awali alikuwa akivunja amri ya sita na mrembo Naya  Rivera…

Na badala yake alifunguka hivi ”Mimi nadhani  udadisi utakuuwa . Sijui hata cha kusema, Ryan. Kwa nini unanifanyia hivi? Nitakwambia wakati hatupo hewani. Nakuamini. Nimekujua kwa kitambo kirefu. Sijui itakuaje kwa mamilioni ya watu wanaotusikiliza hivi sasa”.

Hitmaker huyo wa Problem na Big sean wamekuwa wakizungumziwa na vyombo vingi vya habari  siku za hivi karibuni hasa kutokana na ukaribu uliopo baina yao huku tukio la Utoaji wa Tuzo za MTV Video Music Awards likichochea tetesi hizo hasa kutokana na mahaba niue waliyokuwa wakionyeshana siku hiyo.

Ariana Grande  na Big Sean

Ariana Grande akitaniana na Big Sean wakati wakiingia kushuhudia utoaji wa Tuzo za MTV Video Music Awards

Big Sean na Ariana MTV VMA

Big Sean akiwa ameshikana mikono na Ariana Grande ..

 

Enzi Hizooo!!!  Big Sean akiwa na zilipendwa wake  Naya Rivera

Enzi Hizooo!!! Big Sean akiwa na zilipendwa wake Naya Rivera

 

 

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s