SHULE ZAFUNGWA NIGERIA KWA HOFU YA EBOLA

NigeriaShule zote nchini Nigeria zilizokuwa zianze muhula mpya jumatatu zimeagizwa kuahirisha siku ya kufungua muhula hadi oktoba tarehe 13 kama moja wapo ya njia za kuzuia kuenea kwa viusi vya Ebola.

Waziri wa elimu Ibrahim Shekarau ameamuru zisifunguliwe ili kuwapa walimu mafunzo jinsi ya kushughulikia ugonjwa huo. Inatarajiwa angalau wafanyakazi wawili kila shule katika zile za umma na za kibinafsi watapata mafunzo maalum ya ugonjwa huu kufikia septemba 15 ambapo itahusisha jinsi ya kuutambua dalili na jinsi ya kujikinga.

Watu watano wamekufa kufuatia mambukizi ya homa ya ebola nchini Nigeria .Ugonjwa huu uliozuka Magharibi mwa Afrika hasa Guinea, Liberia na Sierra Leone umewauwa zaidi ya watu 1,400 .

Ulienea Nigeria nchi iliyo na watu wengi zaidi mwezi Julai baada ya mtu aliyekuwa na virusi kutua nchini humo kutoka Liberia.

-bbcswahili.com

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s