ANGEL DI MARIA ATUA OLD TRAFFORD

Angel Di Maria

Di Maria akikabidhiwa jezi na kocha mkuu wa Manchester United, Loius Van Gaal

Kiungo  wa kimataifa wa Argentina, Angel Di Maria ametia saini mkataba wa miaka mitano kukitumikia kikosi cha mashetani wekundu klabu ya Manchester United kwa ada ya uhamisho wa pauni  milioni 59.7 akitokea Real Madrid ya Hispania.

Di Maria mwenye umri wa miaka 26 anakuwa mchezaji wa pili wa United kulipwa mshahara mnono zaidi akiwa nyuma ya straika Wayne Rooney.

”Nina furaha kujiunga na Manchester United. Nimeufurahi muda wangu nikiwa Hispania na kulikuwa na vilabu vingi vilivyokuwa vinanihitaji, lakini United ni klabu pekee ambayo imenifanya niondoke Madrid” . Luis Van Gaal ni kocha mzuri sana mwenye rekodi nzuri ya mafanikio, kila mmoja wetu anapaswa kuirudisha hii klabu kileleni ilipokuwa. alisema Di Maria.

Nae kocha mkuu wa United, Louis Van Gaal alikuwa na haya ya kusema, ”Angel ni kiungo wa kimataifa, lakini muhimu zaidi yeye ni mchezaji wetu. Hakuna mashaka na kipaji chake asilia”.

 

 

 

 

   

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s