MAN CITY YAIFUMUA 3 – 1 LIVERPOOL

Stevan Jovetic

Straika wa Manchester City, Stevan Jovetic akishangilia kwa kuteleza baada ya kufunga bao la pili dhidi ya Liverpool

Kocha mkuu wa manchester City, Manuel Pellegrini hataki mchezo kabisa hasa linapokuja suala zima la kugombea pointi tatu muhimu katika msimu huu mpya wa ligi kuu ya England  baada ya kuwaangushia kichapo cha bao 3 – 1 majogoo wa jiji la London ‘Liverpool’ katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la  Etihad usiku wa jana.

City ndio walikuwa wa kwanza kuzifumania nyavu za Liverpool kupitia mchezaji wake Stevan Jovetic ambaye alitupia goli mnamo dakika ya 41 na 55 pamoja na Sergio aguero aliyepachika bao la tatu mnamo dakika ya 69 kabla ya beki  Pablo zabaleta kujifunga wakati akiwa kwenye harakati za kuokoa mpira na kuiwezesha Liver kupata bao moja la kufutia machozi mpaka mchezo unamalizika.

Kwa matokeo hayo yanaiweka Man City kileleni ikiwa na alama 6 sawa sawa na Spurs, Chelsea na Swansea ambao hawajapoteza mchezo wowote tangu kuanza kwa ligi hiyo ngumu huku wakiwa tayari wameshacheza michezo miwili kila mmoja.

Sergio Aguero

Sergio Aguero akipiga shuti lililozaa goli langoni mwa Liverpool

Pablo zabaleta

Kipa wa City akijaribu kuokoa mpira uliopigwa na Pablo zabaleta lakini maji yalizidi unga na kujikuta ukiingia kiulaini golini mwao .

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s