VAN GAAL NGOMA NGUMU, ALAZIMISHWA SARE YA 1 – 1 NA SUNDERLAND, SPURS YAILOWESHA 4 – 0 QUEENS PARK

Juan Mata

Pichani ni Mchezaji wa United ‘Juan Mata’ akiweka mpira wavuni kwenye lango la Sunderland

Kikosi cha Louis Van Gaal, klabu ya Manchester United ikiwa ugenini imelazimishwa sare ya 1 – 1 na Sunderland katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la Stadium of Light hapo jana.

Kiungo wa United, Juan Mata  aliweza kuipatia timu yake bao la kuongoza kabla ya Jack Rodwell kuisawazishia Sunderland mnamo dakika ya 30′ kipindi cha kwanza na matokeo kumalizika kwa suluhu ya moja moja, huku Tom Cleverley na Ashley Young wakijikuta wakimaliza mchezo huo kwa kuonyeshewa kadi ya njano.

Kocha mkuu wa United, Luis Van Gaal akiteta jambo na kocha msaidizi Ryan Giggs

Kocha mkuu wa United, Luis Van Gaal akiteta jambo na kocha msaidizi Ryan Giggs

Tangu kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu ya England(EPL), United  imeshindwa kabisa kuonyesha makali yake katika michezo miwili na kujikuta ikipoteza pointi tatu muhimu katika mchezo wake wa kwanza wa ufunguzi baada ya kupokea kichapo cha bao 2 – 1 dhidi ya Swansea.

Mchezo mwingine uliokuwa wa kukata na shoka ni ule wa Tottenham Hotspur waliowakaribisha nyumbani Queens Park Rangers na kuipatia kipigo kitakatifu cha jumla ya mabao 4 – 0 kupitia wachezaji wake Nacer Chadli aliyetupia magoli mawili, Eric Dier, pamoja na Emmanuel Adebayor.

1408889944164_wps_1_Tottenham_v_QPR_premier_l

Kiungo wa Sours, Nacer Chadli(Kushoto) akipiga kmpira kwa kichwakuelekea golini mwa Queens Park ulioweza kuzaa matunda

 

 

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s