ALIYEKUWA BOSI WA MAREHEMU 2PAC SHAKUR ‘SUGE KNIGHT’ AJERUHIWA VIBAYA KWA RISASI

Marion Suge Knight

Marion Suge Knight

Huenda ile nadharia ya mtu aliyehusika na mauaji ya Rapa 2pac Amaru Shakur ikawa bado haijafutika vichwani mwa watu baada ya aliyekuwa Meneja wake  na mmiliki wa lebo ya Death Row ‘Marion Suge Knight kupigwa risasi mara mbili eneo la tumboni na mkononi na watu wasiojulikana.

Shambulio hilo lilitokea mishale ya saa 7 usiku katika eneo la Sunset strip Hotspot wakati Suge Knight akitokea kwenye Pre Party ya MTV Video Music Awards iliyokuwa ikishereheshwa na Chris Brown kwenye klabu ya usiku ya  10ak iliyopo magharibi mwa mji wa Hollywood nchini Marekani .

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ umedai kwamba baada ya Suge Knight kushambuliwa alijitaidi kujikokota kabla ya polisi wa doria kumwona na kumkimbiza katika hospitali ya Cedars-Sinai ambapo inaelezwa amefanyiwa upasuaji akiwa miongoni mwa watu watatu walioshambuliwa.

Itakumbukwa kuwa Suge Knight ni miongoni mwa watu waliohisiwa kuhusika kwa namna moja ama nyingine kupanga njama za mauaji ya Rapa 2pac Shakur  yaliyotokea Septemba 7 mwaka 1996 mjini Las Vegas Nevada wakati wakitokea kwenye pambano la masumbwi la bondia Mike Tyson.

 

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s