Staa wa miondoko ya Pop Duniani na Mshindi wa Tuzo ya Grammy, Christina Aguilera amejifungua salama mtoto wa kike kwa njia ya upasuaji Agosti 16 mwaka huu kwenye hospitali ya Cedars-Sinai Medical Center mjini Los Angels .
Aguelera mwenye miaka 33, amempa binti yake huyo jina la ”Summer Rain Rutler” aliyezaa na Matt Rutler akiwa ni mtoto wake wa pili toka kwa wanaume wawili tofauti ukiacha yule wa kiume aitwae Max ambaye alizaa na mtalaka wake Jordan Bratman miaka sita iliyopita.