VAN GAAL AKARIBISHWA EPL KWA KIPIGO CHA BAO 2 – 1 TOKA KWA SWANSEA

1408192061416_wps_33_Swansea_City_s_Ki_Sung_yu

Sung-Yueng wa Swansea akishangilia pamoja na wachezaji wenzake baada ya kupachika bao la kwanza

Kocha muholanzi Louis Van Gaal anayekinoa kikosi cha Mashetani wekundi ‘Manchester United’ amekaribishwa kwenye ligi kuu ya England(EPL) kwa kipigo cha bao 2 – 1 dhidi ya Swansea katika mtanange uliochezwa kwenye  dimba la Old Trafford ikiwa ni mara ya kwanza kufungwa nyumbani katika mechi ya ufunguzi tangu ifanye hivyo mwaka 1972.

Swansea City ndio waliokuwa wakwanza kuzifumania nyavu za Man United kupitia mchezaji wao Sung-Yueng kabla ya Straika Wayne Rooney kusawazisha mnamo dakika ya 53′ ya kipindi cha pili cha mchezo hata hivyo bahati haikuwa yao baada ya  Gylfi Sigurdsson kuipatia Swansea bao la pili na la ushindi.

Rooney

Straika wa Manchester United, Wayne Rooney akishangilia bao la kusawazisha

Mchezo mwingine ni ule uliowakutanisha washika mtutu wa jiji la London, Arsenal walioipa kibano cha goli  2 – 1 Crystal Palace kupitia wachezaji wake Laurent Koscielny na Aaron Ramsey  wakati bao pekee la Palace likifungwa na Brede Hangeland.

Matokeo mengine ni Leicester United iliweza kutoka suluhu ya bao 2 – 2 dhidi ya Everton,  Tottenham ikimtandika bao  1-0 West Ham wakati Stoke ikichezea kichapo cha bao 0 – 1 toka kwa Aston Villa, Queens Park ikikubali kipigo cha bao 1 toka kwa  Hull City na Wenyeji West Bromwich ikilazimishwa sare ya 2 – 2 na Sunderland.

1408196921827_Image_galleryImage_epa04356355_Swansea_City_

Mchezaji wa Swansea, Gylfi Sigurdsson akishangilia mara baada ya kuifungia timu yake bao la pili na la ushindi

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s