HAKUNA EBOLA TANZANIA

Hakuna Ebola TanzaniaTanzania imesema haina mgonjwa aliyethibitishwa kuwa na ugonjwa wa Ebola.  Kauli hiyo inakuja baada ya kufanyiwa uchunguzi kwa wagonjwa wawili waliotiliwa shaka kuwa na ugonjwa huo.

Waziri wa Afya wa Tanzania Seif Rashid ameiambia BBC, wagonjwa hao waliohisiwa kupata maambukizo kutokana na dalili za awali, ni wa kutoka Benin na Mtanzania, lakini vipimo vimeonesha hawana maambukizo hayo.

Amesema tayari eneo maalumu limetengwa kwa ajili ya kufanyia uchunguzi wagonjwa wanaotiliwa shaka kuwa na ugonjwa huo. Mafunzo yametolewa pia kwa wataalamu watakao hudumia wagonjwa iwapo watatokea.

Vifaa maalumu vitakavyotumiwa na watoa huduma katika kuhudumia wagonjwa, vimewekwa pia. Wizara ya Afya ya Tanzania inaongeza uwezo wa kufanya uchunguzi, katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, ambao wasafiri wengi kutoka nje huutumia.

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s