DIAMOND AWACHANA LAIVU WANAODAI ANAMTUMIA WEMA KIMASLAHI

Diamond na wemaMbongo Fleva, Naseeb Abdul AKA Diamond amewapa jibu wale wote wanaomtupia lawama na kudai kuwa anamtumia kimaslahi nyonga mkalia ini wake, Wema Isaac Sepetu hali iliyopelekea kuanzishwa kwa kampeni iliyopewa jina la #BringBackOurWema kwa wafuasi wa nyota huyo maarufu kama Team Wema.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram wenye wafuasi zaidi ya laki na nusu,  Diamond aliandika “!Nafkiri ningewaona kweli Mnaakili na Mapenzi ya dhati kwa Msanii wenu… kama mngemshauri apunguze Mashoga wapenda anasa na apunguze Stareh zisizo na Faida, wenda ingemsaidia Pesa kuzitumia kwenye kufanya kazi na kuleta maendeleo badala ya kuwapa viwanda vya pombe… Mimi kama bwana, wajibu wangu ni kuhakikisha Mpenzi wangu anakula vizuri, anavaa vizuri, analala vizuri, na kumuwezesha mtaji wa kufanyia kazi…. Waswahili wanasema Mchungaji bora anatakiwa kuhakikisha anampeleka Ng’ombe wake Kwenye Maji safi….ila yeye ng’ombe mwenyewe ndio anatakiwa aamue kunywa maji!!!!! Au mnataka nikishampa mtaji niache kufanya na show tena na kuigiza nimuigizie mie ???? Nisiende Studio nikae dukani nimuuzie mie????.. ni juhudi zako kwanza!… leo hii mimi Hata ningepewa Mamilioni ya mamilioni kama nisingekuwa na moyo wa mie mwenyewe kwanza kutaka kujituma na kupenda kufanya kazi yangu nisingefikia hapa nilipo!….Mxieeeeeeeew!�� Kama nimekuchefua Lamba ndimu Usitapike” hata hivyo hapo baadae aliufuta ujumbe huo.

 

 

Advertisements

5 thoughts on “DIAMOND AWACHANA LAIVU WANAODAI ANAMTUMIA WEMA KIMASLAHI

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s