HALI TETE : EBOLA YAHOFIWA KUINGIA TANZANIA, WAWILI WASADIKIWA KUWA NAO

Ebola

Watu wawili wanaosadikiwa kuwa na ugonjwa wa Ebola wamefikishwa katika kituo maalum kilichotengwa na serikali kwa ajili ya waathirika wa ugonjwa huo kilichoko Temeke jijini Dar es salaam.

Kwa mujibu wa Radio One Stereo imesema kwamba baada ya kufika kituoni hapo  ilifanikiwa kumkuta mtu mmoja Raia  wa Benin anayesadikiwa kuwa na ugonjwa huo ambaye alifikishwa hapo kutoka kwenye hospitali ya AMI aidha imeshuhudia gari la wagonjwa likiingia katika kituo hicho likitokea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere ambalo lilimshusha mtu mmoja akitokea uwanjani hapo huku akitokwa na damu puani akijiziba kwa pamba.

Akizungumzia kutengwa kwa eneo hilo, kaimu mganga mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Dkt. Grace Maghembe amesema bado serikali inaendelea na maandalizi katika eneo hilo na kuthibitisha kupokelewa kwa Raia  wa Benin na wakati akiendelea kutoa maelezo hayo aliwasili mtu mwingine anayehofiwa kuwa na maambuzi ya ugonjwa huo alipofikishwa kwenye kituo hicho.

Katika hatua nyingine abiria wanaowasili katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam wameanza kuchunguzwa kama wanamaambukizi ya ugonjwa huo au lah.

Ofisa afya mfawidhi wa uwanja wa ndege Dkt. George ndaki amesema kwa sasa uwanja umepata vifaa ili kujikinga na ugonjwa huo wakati wa ukaguzi.

Chanzo : ITV

Advertisements

One thought on “HALI TETE : EBOLA YAHOFIWA KUINGIA TANZANIA, WAWILI WASADIKIWA KUWA NAO

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s