Kocha mpya wa Klabu ya Wekundu wa Msimbazi ”Simba Sc”, Mzambia Patrick Phiri ametua nchini leo hii Jumatano Agosti 13 katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam.
Phiri ambaye amekuja kukamilisha makubaliano ya mkataba wa mwaka mmoja kuwanoa wekundu hao wa Msimbazi kwa msimu ujao wa ligi kuu ya Soka Tanzania Bara amenukuliwa akisema amekuja kuleta ubingwa kwa Timu ya Simba.
Kocha huyo Mzambia amesema amekuwa akiifuatilia Simba kwa kipindi kirefu na ameiona Timu hiyo ikiandamwa na majanga ya kufanya vibaya lakini anaamini ujio wake ndani ya klabu hiyio utafuta majanga hayo na kurejesha furaha Msimbazi.
Katika uwanja wa ndege wa Mwalimu JK Nyerere, mashabiki wa klabu ya Simba wamejitokeza kwa wingi kumpokea kocha wao na kuwaduwaza wasafiri wanaotumia uwanja huo baada ya kupiga ngoma na kucheza kwa furaha.
Patrick Phiri anakuwa kocha wa Tatu wa Simba kuifundisha timu hiyo kwa vipindi vitatu tofauti akiungana na Abdallah Kibadeni na Julio ambapo alianza mwaka 2003 hadi 2005 kisha akarejea tena 2008 hadi 20011 na katika vipindi vyote hivyo ametwaa ubingwa pasipo kufungwa hata mechi moja.

Kocha wa Simba(Katikati), Patrick Phiri (Katikati) akitoka nje ya viunga vya uwanja wa ndege wa Mwalimu na viongozi wa klabu ya Simba
Namwaminia sana
Hawa simba wamejichanganya watafungwa hadi basi Sitaki tena kushabikia simba bora nirudi kushabia polisi tabora huenda ikapanda super ligi mwakani nihaya2 By, PAULO FROM TABORA