MUIGIZAJI ROBIN WILLIAMS AFARIKI DUNIA AKIWA NA MIAKA 63

Robin Williams

Robin Williams

Muigizaji na mvunja mbavu mkongwe wa Hollywood aliyewahi kutamba kwenye komedi kama vile Mrs.Doubtfire, Dead Poets Society pamoja na Good Morning, Vietnam, Robin Williams amekutwa amefariki nyumbani kwake eneo la Tiburon California akiwa na umri wa miaka 63 huku Polisi wakidai  kifo chake huenda kimesababishwa na kujiua.

Inaelezwa kuwa miezi michache kabla ya kifo chake, Williams aliwahi kukiri kupatiwa matibabu na kituo cha ushauri tiba cha Hazelden Addiction Treatment Center kilichopo Lindstrom mjini Minnesota baada ya kuwa muathirika wa  dawa za kulevya na kusumbuliwa na  msongo wa mawazo.

Mke wa Marehemu Bi. Susan Schneider amenukuliwa akisema ”Nimempoteza Mume na Rafiki yangu, wakati Dunia ikiwa imempoteza msanii kipenzi cha wengi. Nimehuzunishwa”.

Salamu za pole zimeendelea kutolewa kutoka kwa watu mbalimbali mashuhuri Duniani  na wale waliowahi kufanya kazi na Williams akiwemo mchekeshaji mwenzake ‘Steve Martin’ ambaye ameandika ujumbe mzito kwenye ukurasa wake wa Twitter, ”I could not be more stunned by the loss of Robin Williams, mensch, great talent, acting partner, genuine soul.”.

Marehemu ameacha mjane na mtoto mmoja wa kike aitwaye Zelda Williams . “I love you. I miss you. I’ll try to keep looking up.” aliandika Zelda

Robin Williams enzi za uhai wake akiwa na binti yake Zelda

Robin Williams enzi za uhai wake akiwa na binti yake Zelda

 

 

 

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s