SIMBA YAVUNJA MKATABA NA KOCHA WAKE ZDRAVKO LOGARUSIC

ZdravkoLogarusic

Zdravko Logarusic

SIMBA SC imevunja Mkataba na kocha wake, Mcroartia Zdravko Logarusic siku moja tu baada ya timu hiyo kufungwa mabao 3-0 na ZESCO ya Zambia katika mchezo wa kirafiki jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

 Rais wa Simba SC, Evans Aveva amesema kwamba Logarusic amevunjiwa Mkataba kwa kukiuka masharti ya mwajiri wake na sasa Nahodha wa zamani wa klabu hiyo, Suleiman Abdallah Matola ‘Osama’ aliyekuwa Msaidizi wa Loga, ndiye anakuwa kaimu kocha Mkuu hadi atakapopatikana mwalimu mwingine.

Loga ambaye aliongezewa Mkataba wa mwaka mmoja mwezi uliopita- inadaiwa amefukuzwa kwa sababu za kinidhamu na kikubwa ni kuwatolea maneno yasiyofaa wachezaji.

 Inaelezwa Loga alifikia hatua ya kuwadharau na kuwatolea maneno yasiyofaa hadi viongozi wa klabu hiyo.

 Loga anaondoka Simba SC baada ya kuiongoza katika mechi 21 tangu Desemba mwaka jana, kati ya hizo akishinda nane, sare tano na kufungwa nane.

 Loga aliyerithi mikoba ya Mfaransa, Patrick Liewig aliikuta Simba SC bado ipo kwenye mbio za ubingwa msimu uliopita, lakini mwishowe ikamaliza nafasi ya nne nyuma ya Mbeya City, Yanga SC na Azam FC mabingwa.

-BinZubery.Com

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s