PICHA ZA KILICHOJIRI KWENYE TAMASHA LA USIKU WA MATUMAINI UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM

Hatimaye Siku iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa burudani mbalimbali imefikia kilele chake  Uwanja wa Taifa kulipofanyika  Tamasha lililopewa jina la usiku wa  matumaini ambapo watu mashuhuri wakiwemo wabunge, wacheza filamu, wanamuziki, madairekta pamoja na mabondia wameweza kukata kiu za Watanzania wazalendo waliohudhuria Tamasha hilo.

Mechi baina ya waheshimiwa Wabunge mashabiki wa Yanga na Simba ilionekana kuwa kivutio kikubwa baada ya wabunge wa Yanga kuwalowesha Simba jumla ya mabao 3 – 2, kama hiyo haitoshi mpambano wa masumbwi uliowakutanisha mastaa wa filamu, JB na Cloud ambapo mpaka mwisho wa mpambano JB AKA Bonge la bwana aliweza kuibuka mbabe wakati kwa upande Mada Maugo alifanikiwa kumchapa  mpinzani wake Thomas kwa Knok Out.

b4

Wasanii wa filamu Bongo Movie, Cloud wa kwanza kushoto akimsukumia konde zito mpinzani wake Jaccob Steven AKA JB

 

b2

Bondia Mada Maugo akikwepa konde kutoka kwa Thomas mashali

b3

Leo mjini hakutalalika Mwanamasumbwi mwenye mbwembwe nyingi kupita maelezo ”Mada Maugo” akiwa amebebwa juu na mashabiki baada ya kumtembezea kichapo cha mbwa mwizi mpinzani wake Mashali

b1

First Runner wa kundi la Mapacha wa Tatu, Khalid Chokoraa(Wa kwanza Kushoto) akimtembezea kipigo hatari mpinzani wake Said memba katika mpambano wa Raundi 4

B5

Wasanii wa muziki wa Bolingo na Hip-Hop mara baada ya kuwasili uwanja wa taifa kwenye Tamasha la Matumaini. Kutoka kushoto ni memba wa Mapacha 3, Jose Mara, Kimbunga Mchawi, Chokoraa pamoja na meneja wao Hamis Dakota

B6

Mkurugenzi wa Global Publishers, Eric Shigongo akitoa neno wakati wa ufunguzi wa Tamasha la matumaini

W1

Waheshimiwa Wabunge wa Yanga na Simba wakiingia Dimbani tayari kabisa kwa mpambano

B7

sehemu ya watu waliohudhuria Tamasha la Matumaini

W5

Waamuzi waliochezesha mchezo baina ya wabunge wa Yanga na Simba

W4

Mashabiki nazi wa Simba na Yanga wakiwashangilia wabunge

W3

Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete akiwapa dole mashabiki

 

W6

Kikosi hatari cha wabunge wa Yanga kilichowatandika bao 3 – 2 wabunge wa Simba

W7

Kikosi cha wabunge mashabiki wa Simba kilichochezea kipigo

W8

Mwamuzi wa mchezo akiwa muongozo makapteni wa Simba na Yanga

W2

Ridhiwani Akifanya mambo yake

W9

Naibu waziri wa fedha, Mwigulu Nchemba akipiga shuti kali kuelekea langoni mwa Simba

W11  W10

W13

Ridhiwani Kikwete alishindwa kuvumilia ikabidi awatupie jezi yake mashabiki ibaki kama ukumbusho

W12

Shabiki damu damu wa Mwigulu Nchemba akimpongeza kwa kile alichokifanya uwanjani

 Picha kwa hisani ya Michuzi Matukio

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s