TAIFA STARS YATOLEWA KWA KIPIGO CHA BAO 2 – 1 TOKA KWA MSUMBIJI

Mshambuliaji wa TP Mazembe na Timu ya Taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta akikokota mpira kuelekea langoni mwa msumbiji

Mshambuliaji wa TP Mazembe na Timu ya Taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta akikokota mpira kuelekea langoni mwa msumbiji

Ama Kweli sio la kufa halisikii dawa.Timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars imekubali kichapo cha mabao mawili kwa moja kutoka kwa wenyeji wao Msumbiji katika mchezo wa  marudiano wa kuwania kuingia katika hatua ya makundi uliochezwa jioni ya leo mjini maputo nchini Msumbiji na hivyo kuzimwa mbio zake za kutafuta tiketi ya kucheza hatua ya makundi kwa ajili ya kusaka tiketi ya michuano ya Afrika(AFCON) mwakani nchini Morocco.

Mtanange huo ulikuwa mkali na wa kusisimua ukichezwa katika uwwanja wa Simpeto mjini Maputo ambapo Stars hadi mapumziko ilikuwa nyuma kwa goli moja kwa bila lakini kipindi cha pili ilipoingia iliweza kucheza vizuri ambapo mshambuliaji hatari wa TP Mazembe, Mbwana Samatha akaisawazishia Stars na kufanya matokeo kusomeka moja moja .

Hata hivyo wenyeji mambas Msumbiji waliweza kuandika bao la pili katika kipindi hicho cha pili baada ya mpira wa adhabu ndogo kupigwa na kwenda moja kwa moja kimyani na kumuacha mlinda mlango Deogratius Munishi ”DIDA” asijue la kufanya. Kikosi cha Stars kinatarajia kurejea nyumnbani hapo kesho milango ya saa moja jioni kwa majira ya Tanzania

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s