MICHAEL WAMBURA AFUTWA UANACHAMA SIMBA SPORTS CLUB

Michael WamburaMkutano mkuu wa klabu ya wekundu wa Msimbazi ”Simba” umemfuta uanachama aliyekuwa mgombea wa nafasi ya urais wa klabu hiyo katika uchaguzi mkuu uliopita, Michael Richard Wambura na wenzake 70 kwa madai ya kupeleka masuala ya soka kwenye mahakama za kawaida za kisheria kinyume na taratibu za mchezo wa soka.

Mkutano huo uliokuwa na agenda 13 ulihudhuriwa na idadi kubwa ya wanachama ulioanza saa 4 asubuhi katika bwalo la maafisa wa polisi na kuongozwa na Rais mpya wa klabu hiyo Evans Eliaza Aveva ambaye aliwataka wanachama kujadili hatma ya wambura na wenzake ambao kwa nyakati tofauti wamedaiwa kuishtaki klabu hiyo katika mahakama kinyume na taratibu za mchezo huo.

Wambura aliyewania nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu uliopita, aliondolewa katika kinyang’anyiro hicho kwa madai ya kufanya kampeni kabla ya muda wake, aliwahi kuishtaki Simba mwaka 2010 katika mahakama za kawaida za kisheria huku wanachama wengine 70 wakidaiwa kufungua kesi mahakama kuu kanda ya Dar es salaam baada ya kutorizishwa na maamuzi ya kamati ya rufani ya uchaguzi ya TFF ya kumuondoa Wambura katika uchaguzi wa mwaka huu.

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s