MBUNGE WA TABORA MJINI ‘ISMAIL ADEN RAGE’ APATA AJALI MBAYA YA GARI AKIELEKEA DODOMA

OLYMPUS DIGITAL CAMERA

Aden Rage

Watu watano akiwemo mbunge wa Tabora mjini, Mheshimiwa Ismail Aden Rage wamenusurika kifo baada ya gari walilokuwa wakisafiria kutoka Tabora kwenda Dodoma kupinduka katika eneo la Chigongwe nje kidogo ya mji wa Dodoma

Imeelezwa kwamba Mheshimiwa Mbunge alikuwa akitokea jimboni kwake Tabora mjini na alikuwa akielekea mjini Dodoma ambapo dereva wa gari lake alikuwa akijaribu kulipita lori lililokuwa mbele yao lakini ghafla lori hilo likaingia katikati ya barabara na hivyo kumlazimu dereva wake aliyefahamika kwa jina la John Honya  kulitoa gari pembeni mwa barabara ambapo palikuwa na korongo lililopelekea gari lao kuruka umbali wa takribani mita 15 na kisha kupinduka kabla ya kukimbizwa katika hospitali ya rufaa mkoani Dodoma.

Katika gari hilo kulikuwa na watu watano, wanne wanaume na mmoja wa kike huku mganga mkuu wa hospitali hiyo akithibitisha hali za majeruhi kuendelea vizuri na muda wowote wanaweza kuachiliwa.

Endelea kutembelea Larrybway91 kwa ajili ya   picha  za ajali hiyo pia unaweza ukatufollow kwenye instagram http://instagram.com/larrybwaythebankroller na katika Twitter @LARRYBWAY 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s