MWANARIADHA USAIN BOLT AISAIDIA JAMAICA KUSHINDA MBIO ZA MITA 400 JUMUIYA YA MADOLA

Usain Bolt

Usain Bolt akishangilia kwa staili ya aina yake mara baada ya mbio kumalizika na kufanikiwa kushinda

Bingwa wa mbio za mita 100 Duniani mjamaica Usain Bolt amelisaidia Taifa lake kunyakua medali ya dhahabu katika fainali za mita 400 za mbio za kupokezana vijiti  hapo jana kwenye uwanja wa Hampden Park mjini Glassgow nchini Scotland.

Awali mwanariadha huyo alikaririwa na vyombo vya habari kwa kuponda mashindano hayo lakini amelazimika kukana matamshi hayo na kudai kuwa alinukuliwa vibaya ambapo nusura timu ya Jamaica ishindwe baada ya kiongozi wa mbio hizo Kemar Bailey-Cole kuumia paja lakini mambo yalikwenda vizuri.

Bolt amesema kuwa alikuwa na wasiwasi kuhusu Kemar na kubainisha kuwa siku zote amekuwa akifuata ushauri waliopewa na kocha wao wa kupigana hadi mwisho kwa ajili ya kulitetea Taifa.

Mbio hizo zimekuwa na ushindani mkubwa kutokana na wanariadha nyota kung’arisha michuano hiyo na kushangiliwa na mashabiki lukuki waliofika uwanjani hapo huku Bolt akikiri bado anakazi ya ziada .

Bolt

Bolt Commonwealth

Bolt akipata uselfie na mashabiki wa Jamaica

Bolt Jamaica

Nani kama Bolt

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s