2FACE AWAKIMBIZA KWENYE CHATI ZA BILLBOARD

2faceMuziki wa Nigeria umeendelea kupasua anga za kimataifa kufuatia albamu mpya ya hitmaker wa African Queen, 2Face Idibia inayoitwa ” The Ascension” kutajwa na jarida la Billboard kama albamu iliyofanya vizuri sokoni katika wiki ya kwanza ikikamata nafasi ya 12.

The Ascension iliyotoka Julai 21 mwaka huu chini ya lebo ya 960 Music Group ikiwa ni albamu ya sita kwa 2face, imeweza kuweka rekodi ya kuwa albamu ya kwanza kutoka Nigeria kukamata nafasi za juu kwenye chati za Billboard zilizotolewa hapo jana(Julai 31).

2face amewashukuru  mashabiki na wale wote waliomsapoti kwa namna moja au nyingine sambamba na kupata pongezi za nguvu  kutoka kwa mama watoto wake, Annie Macaulay-Idibia kupitia ukurasa wake Instagram

”I Am Screaming thank YOU JESUS!!!! This is the 1st time EvER In the world, any Nigerian artist achieved this!!! Record-Breaking! 2face Idibia’s ‘The Ascension’ Album Is Currently The 12th Top Selling Album In The World – Music ” aliandika Annie

Vigezo muhimu vinavyozingatiwa na Billboard katika kupata albamu zinazouza zaidi ni pamoja na kutazama mauzo ya albamu husika, watu wanaoipakua mtandaoni, muda wa hewani kwenye redio, ziara(Touring) na muingiliano wake kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kama vile Facebook, Twitter, Vevo, Youtube, Spotify na mengineyo.

2Face-Idibia-billboard-chart

 Chati ya  Billboard ikionyesha albamu zinazokimbiza kwa mauzo sokoni huku ya 2face ikiwa kwenye nafasi ya 12

 

 

 

 

 

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s