MAJANGA YAENDELEA KUITAFUNA LEBO YA MMG, OMARION NAE ATUPWA JELA

Omarion MaybackUpepo mbaya bado umeendelea kuikumba Kambi ya Mayback Music Group inayomilikiwa na Rick Ross baada ya msanii mwingine anayefanya kazi katika lebo hiyo, Omarion, kukamatwa na kutupwa rumande kwa kosa la kukiuka sheria za barabarani.

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ umeripoti kwamba, Omarion alisimamishwa na askari wa barabarani Ijumaa asubuhi(Julai 18) eneo la San Fernando Valley kwa kosa la kupita taa nyekundi pamoja na leseni yake kuwa na kibali cha kukamatwa  kwa kushindwa kuhudhuria mahakamani hapo awali.

Chanzo toka Mayback kimesema Rick Ross anajaribu kujadiliana na maafisa wa polisi ili aweze kumuwekea dhamana msanii wake  kwa makosa yanayomkabili ikiwemo na faini ya dola 20,000.

Omarion anakuwa msanii kinara wa pili kutoka lebo ya Mayback kusekwa jela katika kipindi kifupi tangu Meek Mill ahukumiwe kifungo cha miezi mitatu mpaka sita   baada ya kukiuka masharti aliyopewa na mahakama katika kipindi cha uangalizi.

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s