MESUT OZIL AJITOLEWA KIFUTA JASHO CHAKE KUSAIDIA GHARAMA ZA UPASUAJI KWA WATOTO 23 WA KIBRAZIL

 

Mesut Ozil

Mesut Ozil

Mashindano ya kombe la Dunia yamemalizika nchini Brazil kwa Ujerumani kuibuka bingwa wa michuano hiyo akifuatiwa na mshindi wa pili ambaye  ni Argentina, kama hiyo haitoshi wachezaji wa timu hizo zote  mbili wameamua kutumia posho zao walizolipwa kama kifuta jasho katika kuisaidia jamii.

Kwa mujibu wa mtandao wa Express umesema kuwa, kiungo mshambuliaji wa Arsenal na Timu ya Taifa ya Ujerumani, Mesut Ozil, amejitolea takribani dola milioni 600 za kitanzania katika kusaidia mifuko mbalimbali ya kijamii nchini Brazil huku sehemu kubwa ya fedha hiyo ikienda kulipia huduma ya   upasuaji kwa watoto 23 wa kibrazil.

Ozil ameandika kwenye ukurasa wake wa Facebook, ”Wapendwa Mashabiki, kabla ya kombe la Dunia nilichangia fedha za upasuaji kwa watoto kumi na moja. Ushindi wa kombe la Dunia sio kwa wachezaji 11 bali ni kwa timu yetu yote,  hivyo sasa nimeongeza idadi ya  kuwasaidia wagonjwa 23. Hii ni shukrani kwa ukarimu wa watu wa Brazil”

Timu ya Taifa ya Argentina haikubaki nyuma baada ya kuripotiwa kuchangia takribani milioni 176 za kibongo kwenye kitengo maalum cha watoto wenye tatizo la kansa katika hospitali ya Buenos Aires nchini humo,  ikiwa ni sehemu ya dola milioni 20 walizopewa kama kifuta jasho kwa kuibuka mshindi wa pili wa World Cup.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s