LEBRON JAMES AWAHUZUNISHA MASHABIKI WA MIAMI HEAT BAADA YA KUREJEA KATIKA TIMU YAKE YA ZAMANI

Lebron James

Lebron James

Uhamisho wa mcheza kikapu aliyekuwa akiichezea timu ya Miami Heat, Lebron james, umeonekana kuzua gumzo baada ya mchezaji nyota huyo kuamua kurejea katika timu yake ya zamani ya Cleveland Cavaliers kwa mkataba wa miaka miwili baada ya kuitumikia  Miami katika misimu minne na kuiwezesha kutwaa ubingwa wa NBA mara mbili pamoja na kupata  Tuzo ya MVP mara nne mfululizo.

Maamuzi ya Lebron yameoneka kutowapendeza baadhi ya mashabiki na wachezaji wa Miami akiwemo Dwayne Wade ambaye ameonyesha kusikitishwa na uamuzi  uliofanywa na swahiba wake wakati kwa upande wa Chris Bosh amenukuliwa akisema anadhani bado wanauwezo wa kuwa wapinzani bila ya uwepo wa Lebron.

”Kama Rafiki na mchezaji mwenzangu, Nasikitika kuona ndugu yangu Lebron anaondoka na kuanza safari mpya, alisema Wade. Mwaka 2010, tuliamua kuhamia Miami kwa lengo moja la kutwaa ubingwa na tulifanikiwa. Tulikuwa marafiki tangu mwanzoni tulipojiunga na tuliweka malengo madhubuti katika kipindi cha miaka minne iliyopita.  Ushirikiano wetu daima utakuwa wa kipekee”.

Mashabiki na wapenzi wa Lebron James wategemee kumuona nyota wao huyo akiwa kwenye jezi mpya yenye namba 23 mgongo ambayo ilikuwa jezi yake ya awali kabla ya kuhamia Heat mwaka 2010 na kupewa jezi namba 8.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s