HASHEEM THABEET AWAFUNGUKIA WABONGO WANAOFIKIRIA AMESAHAU KISWAHILI

Hasheem Thabeet

Hasheem Thabeet

Mchezaji nyota wa mpira wa kikapu, Mtanzania Hasheem Thabeet anayechezea timu ya Oklahoma City Thunder ya Marekani, amewatolea uvivu Raia wa Tanzania wanaofikiria amesahau lugha ya kiswahili na kuwatahadharisha wale wanaomuuliza maswali kama hayo kutomsogelea kabisa kwa sababu anajua kiswahili zaidi ya wanavyomfahamu.

Akionekana kukerwa na ishu hiyo, Hasheem ameandika kwenye ukurasa wake wa Facebook kama ifuatavyo, ‘HIVI NI KWELI KUNA WATU WANAISHI TZ WANAFIKIRIA NIMESAHAU KISWAHILI..? YAANI MASWALI KABISA NA WENGINE KUNISIFIA ETI HONGERA UNAKUMBUKA!! AU HUJASAHAU KISWAHILI?? WEWE KAMA UMEZALIWA TZ, UKAKULIA TZ UKINIONA MTAANI UKANIAMBIA UMESAHAU KISWAHILI NAOMBA USIENDELEE KUONGEA NA MIMI = SITOKUELEWA, KWA SABABU NAJUA KISWAHILI ZAIDI YA HIYO LUGHA UTAKAYOKUWA UNAIONGEA WEWE. HEBU PENDENI KWENU. ‪#‎UZALENDO.

 

 

 

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s