UHOLANZI YAITUNGUA BAO 0 – 3 BRAZIL, YAKAMATA MSHINDI WA TATU

Kikosi cha timu ya Taifa ya Uholanzi wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuibuka na ushindi dhidi ya Brazil

Kikosi cha timu ya Taifa ya Uholanzi wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuibuka na ushindi dhidi ya Brazil

Wenyeji wa kombe la Dunia, timu ya Taifa ya Brazil imeendelea kuandika rekodi mbaya ya kufungwa magoli kumi katika michezo miwili iliyopoteza ikiwa nyumbani kwao katika kipindi cha miaka 75 baada ya hapo jana kukubali kichapo cha magoli matatu kwa nunge toka kwa Uholanzi katika mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu. 

Bao la kuongoza kwa Uholanzi lilifungwa na straika wa Manchester United, Robbin Van Persie kwa njia ya mkwaju wa penalti baada ya Aljen Robben kufanyiwa madhambi ndani ya eneo la kumi na nane na beki wa Brazil, Thiago Silva, huku bao la pili likipachikwa na Daley Blind mnamo dakika ya 17 pamoja na Georginio Wijnaldum dakika ya 90 katika mchezo uliochezwa kwenye dimba la Nacional de Brasilia mjini Brasilia.

Wachezaji wa Brazil wakiwa benchi, huku Neymar akishindwa kuvumilia na kuamua kuficha uso wake kwa aibu

Wachezaji wa Brazil wakiwa benchi, huku Neymar akishindwa kuvumilia na kuamua kuficha uso wake kwa aibu

Matokeo hayo yanaifanya Uholanzi  kuwa mshindi wa tatu wa mashindano  ya kombe la Dunia kwa mwaka huu, wakati mshindi wa pili na bingwa wa michuano hiyo akisubiriwa kwa hamu hii leo katika mchezo wa fainali utakaowakutanisha miamba ya soka toka Amerika Kusini na barani ulaya yaani timu ya taifa ya Argentina na Ujerumani  katika mtanage utakaochezwa hii leo kwenye uwanja wa Maracana mjini Rio De Jenairo majira ya saa tano usiku kwa saa za hapa nyumbani.

Katika fainali hizo za 20 za kombe la Dunia, zaidi ya maafisa elfu 25 wa polisi, vikosi vya zima moto pamoja na majeshi yatashirikishwa katika hatua ya kuimarisha ulinzi katika  mji wa Rio De Janeiro.

Rais wa Brazil, Dilam Rouseff anatarajia kuhudhuria fainali hizo katika uwanja wa Maracana akiandamana na marais wengine 9 akiwemo Rais Vlamidir Puttin wa Urusi na kansela Angela Merkel wa nchini Ujerumani   huku takribani meli 25 zitakuwa zinapiga doria ndani ya mji huo na usalama vile vile utaimarishwa  ili mashindano hayo yamalizike yakiwa katika hali ya amani.

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s