LUIS SUAREZ ASAJILIWA NA BARCELONA KWA ADA YA UHAMISHO WA PAUNI MILIONI 75

Luis SuarezLiverpool imethibitisha kumuuza mshambuliaji wao raia wa Uruguay, Luis Suarez kwenda klabu ya Barcelona kwa ada ya uhamisho wa pauni milioni 75.

Suarez amejiunga kuichezea Barcelona kwa mkataba wa miaka mitano. Kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers alinukuliwa akisema ”Luis ni mchezaji mwenye kipaji cha kipekee na namshukuru kwa kipindi chote cha miaka miwili alichocheza katika wakati wangu”

Vile Vile Taarifa toka tovuti ya Liverpool ilikaririwa ikisema ”Liverpool FC imethibitisha kwamba Luis Suarez ataondoka  baada ya makubaliano ya uhamisho yakayoafikiwa na FC Barcelona. Kwa sasa ana ruhusa ya kukamilisha taratibu za kawaida, ambazo zitahitimishwa kwenye uhamisho.

Iliongezea ”Tungupenda kumshukuru Luis kwa mchango wake na -jukumu lake la kuisaidia kuleta ligi ya mabingwa Anfield”.

”Kila mtu wa klabu ya Liverpool anamtakia Luis  na familia yake kila la kheri ya maisha yake ya baadae”.

Hata hivyo Luis Suarez hataruhusiwa kujihusisha na mazoezi ya timu yake hiyo mpya mpaka pale atakapomaliza adhabu inayomkabili ya miezi mitatu baada ya kumuuma meno beki wa Italia, Georgio Chiellini wakati wa mchezo wa kombe la Dunia uliozikutanisha Uruguay na Italia.

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s