MEEK MILL AHUKUMIWA KWENDA JELA MIEZI 6

Meek MillRapa wa MMG, Meek Mill, amekamatwa na polisi usiku wa ijumaa(Julai 11) mjini Philadelphia baada ya kukiuka masharti aliyopewa na mahakama katika kipindi cha uangalizi.

Meek Mill amekumbana na adhabu ya miezi mitatu  mpaka sita jela baada ya waendesha mashtaka kutilia wasiwasi idadi ya matukio ya hivi karibuni ya staa huyo, ikiwa ni pamoja na kuposti picha akiwa na bunduki.

Leo katika mahakama, jaji alimwambia Meek Mill, ”sikutaka kufanya hivi, lakini umenishawishi kufanya hivyo” na kisha akatoa hukumu ya miezi mitatu mpaka sita katika gereza la mjini hapa.

Inaelezwa kuwa mwanasheria wa Meek Mill alijaribu takribani  masaa manne kuwashawishi waendesha mashtaka kutomweka ndani mteja wake lakini ilishindikana.

Meek Mill mwenye miaka 27 alikaririwa akisema kazi yake ya muziki wa Hip Hop  imemsaidia kukidhi mahitaji yake pamoja na familia yake akiwemo mama, dada na mwanae wa kiume sambamba na kutaja  kiasi anachotumia kwa mwezi kufikia dola za kimarekani elfu 80 mpaka 90.

”Ilinichukua miaka 15 kufika hapa nilipo na hukumu hii itaniharibia sana maisha yangu” Meek Mill aliliambia jopo la majaji. 

Watu wa karibu wa rapa huyo waliuambia mtandao wa TMZ kuwa Meek  Mill anafikiria mwendesha mashtaka amemkandamiza kwa sababu anatarajia kuiachia albamu yake mpya ya Dream Worth More Than Money  mwezi septemba mwaka huu.

Wakati hukumu hiyo ikisomwa, huku nje baadhi ya marapa, mashabiki na marafiki wa Meek Mill wameanzisha kampeni maalum mtandaoni iliyopewa jina la FreeMeekMill inayowashinikiza wenye mamlaka kumwachia huru mtu wao huyo.

Davido alipost kwenye ukurasa wake wa Instagram

Davido nae amepost ujumbe huo hapo juu kwenye ukurasa wake wa Instagram,  akishinikiza kuachiwa huru kwa rafiki yake Meek Mill

 

 

 

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s