ALEXIS SANCHEZ ASAJILIWA NA ARSENAL

Alex Sanchez

Alexis Sanchez akiwa ndani ya uzi mpya wa Arsenal

Arsenal imethibitisha kumsajili mshambuliaji hatari wa klabu ya Barcelona na timu ya Taifa ya Chile, Alexis Sanchez,  kwa ada ya uhamisho wa pauni milioni 40.

Sanchez ambaye alifanyiwa vipimo Alhamisi mchana,  uhamisho wake umeweka historia ya kuwa mchezaji wa pili ghali kuwahi kununuliwa na washika mtutu hao wa jiji la London ukiacha ule wa Metsu Ozil uliowagharimu kiasi cha pauni milioni 42.5.

Straika huyo mwenye umri wa miaka 25, ameifungia timu yake ya Taifa  mabao mawili katika michuano ya kombe la Dunia nchini Brazil huku akiweka rekodi nzuri ya kuifungia Barcelona mabao 39 katika mechi 88 alizocheza ndani ya misimu mitatu ya ligi kuu ya Hispania maarufu kama La Liga.

”Nina furaha kujiunga na Arsenal, klabu ambayo ina meneja mzuri, kikosi imara, inayoungwa mkono Duniani kote na yenye uwanja mkubwa London”  Sanchez aliiambia tovuti ya Arsenal

Alexis Sanchez

Alex Arsenal  Sanchez Fly EmiratesASanchez

 

 

 

 

 

 

 

Advertisements

One thought on “ALEXIS SANCHEZ ASAJILIWA NA ARSENAL

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s