”SING’OKI BRAZIL NG’OO” ASEMA SCOLARI

Scolari

Kocha wa Brazil, Luiz Felipe Scolari

Mganga huwa hajigangi, kufuatia dhahama kubwa ambayo iliwakuta wenyeji na waandaaji wa mashindano ya kombe la Dunia, timu ya Taifa ya Brazil   baada ya kupokea kichapo cha mabao 7 toka kwa Ujerumani katika hatua ya nusu fainali, kocha mkuu wa timu hiyo, Luiz Felipe Scolari, amewaomba radhi wananchi wote wa Brazil lakini akasisitiza kamwe hawezi kujiuzulu.

Scolari amenukuliwa akisema ”ujumbe wangu kwa Brazil na mashabiki ni kwamba nilijaribu na kufanya nilichoweza lakini tukaishia pale, tafadhali tusameheane kwa makosa haya, naomba msamaha hatukufika fainali, hili ni pigo na ni wakati mgumu katika maisha yangu ya kazi, hii ni siku mbaya zaidi katika maisha yangu lakini maisha yanaendelea’alisema kocha huyo mwenye umri wa miaka 66.

Mbali ya kocha Scolari kuomba radhi, mwingine ni nahodha wa muda wa kikosi hicho cha Brazil, David Luiz, akiwaomba radhi mashabiki wa timu hiyo kote ulimwenguni.

Luiz ambaye aliitajwa kama nahodha wa muda  baada ya kuchukua nafasi ya nahodha Thiago Silva aliyelimwa kadi mbili za njano na kukosa mchezo huo muhimu kwa Brazil.

”Mtuhieni radhi, sijui tutafanya nini ili tuwaone tena wabrazil wakitabasamu” amesikika akilalamika David Luiz huku akitokwa na machozi na sura yake kubadili kuwa nyekundu kwa uchungu

Ukiona mtu mzima analia, ujue kuna jambo

Ukiona mtu mzima analia, ujue kuna jambo, David Luiz akibubujikwa na machozi

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s