ARGENTINA YAING’OA UHOLANZI NUSU FAINALI

 

Argentina1Nusu fainali ya pili ya michuano ya kombe la Dunia imemalizika kwenye uwanja wa Sao Paulo na ni Argentina na Ujerumani ndio watakaokutana siku ya Jumapili kwenye fainali ya kombe la Dunia katika dimba la  Maracana baada ya kuing’oa Uholanzi kwa mikwaju  minne ya penalti dhidi ya miwili.

Timu hizo zilijikuta zikitoka sare tasa ya bila kufungana katika kipindi cha dakika 120 na hivyo kulazimika kwenda kwenye hatua ya matuta ambapo uholanzi ilijikuta ikiangukia pua kufuatia wachezaji wake wawili Ron Vlaar na Wesley Sneijder kukosa penalti na kuipa  tiketi Argentina ya kutinga fainali.

Mara ya mwisho Argentina kukutana na Ujerumani katika hatua ya fainali ilikuwa mwaka 1990 nchini Italia ambapo Ujerumani magharibi waliweza kuibuka na ushindi dhidi ya Argentina.

Jasper

Kipa wa Argentina, Jasper Cillessen akiwa akijiinamia mara baada ya timu yake kutolewa katika hatua ya matuta

Messi na wachezaji wenzake wakishangalia ushindi

Messi na wachezaji wenzake wakishangalia ushindi

Kipa wa Timu ya Taifa ya Argentina, Romero akishangilia kutinga fainali kufuatia kunyakua mikwaju miwili ya penalti
Kipa wa Timu ya Taifa ya Argentina, Romero akishangilia kwa hisia baada ya kutinga fainali kufuatia kunyakua mikwaju miwili ya penalti

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s