HAIJAWAHI TOKEA !!! BRAZIL YATOLEWA KWA AIBU, YALOWESHWA BAO 7 NA UJERUMANI

 

Klose akishangilia bao lake la 16

Klose akishangilia baada ya kuweka rekodi ya kuwa mfungaji mwenye magoli mengi katika historia ya kombe la Dunia

Mchezo wa nusu fainali ya kwanza wa kombe la Dunia umemalizika kwa mabingwa mara tano na waandaji wa michuano hiyo, timu ya Taifa ya Brazil kukubali kipigo cha kihistoria cha jumla ya magoli saba kwa moja toka kwa Ujerumani katika mtanange uliochezwa kwenye dimba la Estadio Mineirao.

kwa mara ya kwanza Brazil imeweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kufungwa magoli mengi katika hatua ya nusu fainali tangu kuanzishwa kwa mashindano ya kombe la Dunia mwaka 1930.

Katika kipindi cha kwanza, Ujerumani iliweza kuzifumania nyavu za Brazil mara 5, magoli yakifungwa na Thomas Mueller mnamo dakika ya 11′, Miroslav Klose dk ya 23′, Toni Kroos dakika ya 24′ na ya 26′  pamoja na Semi Khedira dakika  ya 29′.

Hali iliendelea kuwa mbaya zaidi kwa Brazil baada ya kuruhusu tena mabao mawili katika angwe ya pili yakifungwa na winga wa Chelsea, andre schuerrle kabla ya kinda   Oscar dos Santos Emboaba Júnior  kufunga goli la kufutia machozi mnamo dakika ya 90 na mchezo kumalizika kwa Ujerumani kuibuka na ushindi mnono wa bao 7 kwa 1 dhidi ya Brazil na kuweza kutinga fainali.

Mshambuliaji mkongwe wa Ujerumani Miroslav Klose aliweza kuandika rekodi mpya ya kuwa mfungaji mwenye magoli mengi katika historia ya kombe la Dunia baada ya goli lake la 16 alilofunga hapo jana kuvunjilia mbali rekodi iliyowekwa na Ronaldo De Lima aliyekuwa na magoli 15.

Kipa wa Brazil, Julio Cesar, akiutazama mpira uliopigwa na mueller ukiingia langoni kwake

Kipa wa Brazil, Julio Cesar, akiutazama mpira uliopigwa na muller ukiingia langoni kwake

  Muller na Klose wakipongezana Klose na Muller wakipongezana

ilibaki kidogo  Beki wa Brazil, Marcelo, achezee ambakati chembe kidevu toka kwa goliati wa Ujerumani Jerome Boateng

ilibaki kidogo Beki wa Brazil, Marcelo, achezee ambakati chembe kidevu toka kwa goliati wa Ujerumani Jerome Boateng

 

Wachezaji wa Ujerumani wakimpongeza Schurrle

Wachezaji wa Ujerumani wakimpongeza Schurrle baada ya kupachika bao la saba

Oscar akipiga shuti kali kuelekea golini kwa Ujerumani lilozaa goli la kufutia machozi kwa Brazil

Oscar akipiga shuti kali kuelekea golini kwa Ujerumani lilozaa goli la kufutia machozi kwa Brazil

Washabiki nazi wa Brazil wakishuhudia timu yao ya taifa ikisulubiwa na Wajerumani

Washabiki nazi wa Brazil wakiwa wamebaki mdomo wazi  wakishuhudia timu yao  ikisulubiwa na Wajerumani

Ilikuwa ni furaha kwa mashabiki wa Ujerumani

Ilikuwa ni furaha na shangwe kwa mashabiki wa Ujerumani

Shabiki huyu wa Brazil alishindwa kuvumilia

Shabiki huyu wa Brazil alishindwa kuvumilia

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s