TIM KRUL AIPELEKA UHOLANZI NUSU FAINALI, ARGENTINA YAITUPA NJE UBELGIJI

Kocha mkuu wa Uholanzi, Van gaal akiwapa muongozi wachezaji wake baada ya dakika 90 kumalizika

Kocha mkuu wa Uholanzi, Van gaal akiwapa muongozi wachezaji wake

Kocha wa timu ya Taifa ya Uholanzi, Luis Van Gaal amekiwezesha kikosi chake kutinga katika hatua ya nusu fainali mara baada ya goli kipa wa timu hiyo, Tim Krul kuibuka shujaa wa mchezo kwa  kuweza kuzuia mkwaju miwili ya penalti toka kwa Bryan Ruiz na Michael Umana wa Costa Rica.

Mchezo mwingine wa hatua ya robo fainali uliochezwa hapo jana ni ulioikutanisha miamba miwili, Argentina iliyoitupa nje Ubelgiji kwa kipigo cha bao moja kwa nunge katika mtanange uliopigwa kwenye dimba la Estadio Nacional De Brasilia,  huku goli pekee na la ushindi kwa Argentina likiwekwa kimyani na mshambuliaji wa klabu ya Napoli ‘Gonzalo Higuain’ na  kuweka rekodi nyingine ya kutinga  hatua ya nusu fainali tangu ifanye ivyo miaka 24 iliyopita.

Straika wa Argentina, Gonzalo Higuain aakishangilia baada ya kupachika bao pekee lililoipa ushindi timu yake  dhidi ya Ubelgiji

Straika wa Argentina, Gonzalo Higuain aakishangilia mara baada ya kupachika bao pekee lililoipa ushindi timu yake dhidi ya Ubelgiji

Kwa matokeo hayo, Argentina pamoja na Uholanzi zimeweza kufuzu katika hatua ya nusu fainali ambapo zinatarajia kuvaana Julai 09 kwenye dimba la Arena De Sao Paulo wakati wenyeji Brazil watapimana nguvu na Ujerumani katika hatua hiyo jumanne ijayo.

Inaelezwa kuwa hizi ni fainali za 20 kufanyika zikiwa tayari zimekwisha shirikisha zaidi ya  mataifa 23,  ukiacha mataifa ya mwaka huu ambayo yamekwishachuana katika hatua ya mikwaju ya penalti na mara ya kwanza mikwaju ya penalti kutumika kwenye kombe la Dunia ilikuwa ni mwaka 1982 katika fainali zilizofanyika nchini Hispania huku takwimu zikionyesha zaidi ya mikwaju 140 imepigwa na zaidi ya asilimia 75 ya mikwaju hiyo imepelekea ushindi kwa timu ambazo zimeshinda mojawapo ikiwa ni Uholanzi.

Tim Krul

Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Uholanzi wakimpongeza kipa wao ‘Tim Krul’ mara baada ya mchezo dhidi ya Costa Rica kumalizika.

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s