BEKI WA COLOMBIA ‘JUAN ZUNIGA’ AZIMA NDOTO ZA NEYMAR, KUKOSA MECHI ZILIZOSALIA ZA KOMBE LA DUNIA

Neymar JrHuenda ikawa habari mbaya zaidi kwa wabrazil na wale wapenzi wa mshambuliaji hatari wa timu ya Taifa ya Brazil na klabu ya Barcelona, Neymar Jr, kufuatia kuvunjika mfupa unaoshikilia uti wa mgongo baada ya kuchezewa rafu mbaya   na beki wa Colombia, Juan Zuniga,  dakika tatu kabla ya mchezo kumalizika ambapo wenyeji Brazil waliibuka na ushindi wa jumla ya magoli mawili kwa moja na kufanikiwa kutinga kwenye  hatua ya nusu fainali.

Neymar ambaye amekwisha ifungia timu yake hiyo ya Taifa magoli manne katika michuano hii ya kombe la Dunia, alishindwa kabisa kumalizia dakika zilizosalia na hivyo kulazimika kuchukuliwa na machela na kukimbizwa hospitali kabla ya daktari wa timu, Rodrigo Lasmar, kuviambia vyombo vya habari nchini humo kuwa straika wao hatoweza tena  kucheza mechi zilizobakia  ambapo ameeleza kuwa huenda ikamchukua  takribani wiki nne au sita kuwa fiti.

‘Sio tatizo kubwa ukizingatia kwamba halihitaji upasuaji, lakini atahitaji kusubiri mifupa ikae sawa  ili aweze kuwa fiti”  Lasmar Alikiambia kituo cha utangazaji cha SportTv

Juan Zuniga

 Beki wa Colombia, Juan Zuniga, akimchezea rafu  Neymar

Neymar Jr

Neymar akiugulia maumivu ndani ya machela

Neymar akiwa amebebwa kwenye machela na watoa huduma ya kwanza

Neymar akiwa amebebwa kwenye machela na watoa huduma ya kwanza

Neymar akiingizwa Hospitalini

Neymar akiwa Hospitalini

Mashabiki wa Brazil wakiwa nje ya hospitali ya Sao Carlos alipolazwa Neymar

Mashabiki wa Brazil wakiwa nje ya hospitali ya Sao Carlos alipolazwa Neymar

Mashabiki wa Brazil wakiwa kwenye  huzuni kubwa nje ya hospitali

Mashabiki wa Brazil wakiwa kwenye huzuni kubwa nje ya hospitali

 

 

 

Advertisements

2 thoughts on “BEKI WA COLOMBIA ‘JUAN ZUNIGA’ AZIMA NDOTO ZA NEYMAR, KUKOSA MECHI ZILIZOSALIA ZA KOMBE LA DUNIA

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s