MAJAMBAZI WASHAMBULIA BASI LA MAHABUSU MIKOCHENI JIJINI DAR ES SALAAM

Baadhi ya mashuhuda wakiwa wanashangaa na kutoamini kutokea kwa tukio hilo linalosemekana lilikuwa kama muvi.

Baadhi ya mashuhuda wakiwa wanashangaa na kutoamini kutokea kwa tukio hilo linalosemekana lilikuwa kama muvi.

Basi la magereza lililokuwa limebeba mahabusu na wafungwa likisindikizwa na askari polisi limeshambuliwa kwa risasi na watu wenye silaha wanaosadikika kuwa ni majambazi eneo la Regency-Hotel Mikocheni, ameeleza shuhuda mmoja.

Watu hao wenye silaha walikuwa wakitokea kwenye kituo cha Nyerere jijini Dar es Salaam walilishambulia basi hilo na kuwajeruhi baadh ya askari.

Mahabusu waliokuwa kwenye basi hilo walianza kushangilia wakati tukio hilo likifanyika, huku ikisemekana kuwa lengo la shambulio hilo ni kuwatorosha mahabusu hao.

Taarifa zinasema kwamba baada ya kushambulia basi hilo, majambazi hao waliweza kukimbia mahali pasipojulikana.

Mpaka sasa hakuna taarifa yoyote kutoka jeshi la polisi na jeshi la magereza kuhusiana na tukio hilo la leo.

 

Gari la Maaskari

Gari la askari likiwa linasindikiza basi hilo la mahabusu, mbale yake ni gari ya wagonjwaa (ambulance).

Upande wa basiUpande wa basi hilo la mahabusu likionekana kupasuliwa kioo na watu hao wanaosadikika kuwa ni majambazi.

Chanzo : Taarifa.co,tz

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s