BONDIA MAYWHEATHER APEWA MIKAUSHO MIKALI NA MKE WA T.I KWENYE TUZO ZA BET

T.I, Floyd Maywheather & TinyBondia Floyd Maywheather amejikuta akiaibika baada ya salamu yake kupotezewa na mke wa Rapa T.I aitwae Tiny,  tukio  lililotokea wakati wa utoaji wa Tuzo za BET zilizofanyika Jumapili iliyopita kwenye ukumbi wa Nokia Theatre  mjini Los Angels, Marekani.

Kitendo kilichoonekana kuungwa mkono na rafiki mkubwa wa Maywheather,  Rapa 50 Cent aliyetumia ukurasa wake wa Instagram kumkanya swahiba wake huyo  kuachana na mke wa mtu

”Now what the f*ck is champ doing with TI woman again. He think shit sweet man DAMN. Leave the man lady alone floyd. I’m call you to talk” aliandika 50 Cent.

Awali T.I na Maywheather waliripotiwa kuingia kwenye ugomvi mkubwa, hali iliyopelekea kurushiana viti sambamba kutoleana maneno machafu ndani ya mgahawa wa FatBurger mjini Las Vegas mwezi mmoja uliopita, huku chanzo cha ugomvi huo  kikitajwa kuwa ni ukaribu uliovuka mipaka kati ya Tiny na mwanamasumbwi huyo asiye na rekodi ya kupigwa.

Hata hivyo mambo yameonekana kukaa sawa baina ya wanandoa hao, baada ya kuonekana wakiwa pamoja usiku wa utoaji wa tuzo hizo.

Picha aliyopost 50 Cent kwenye ukurasa wake wwa Instagram ikimuonyesha mke wa T.I akipotezea salamu ya Maywheather

Picha aliyopost 50 Cent kwenye ukurasa wake wwa Instagram inayomuonyesha mke wa T.I akipotezea salamu ya Maywheather kwenye Red Carpet ya Tuzo za BET 2014

 

T.I na Tiny wakiwa wameshikana mikono huku wakifuatilia kwa makini utoaji wa Tuzo za BET

True love Never Die! T.I na Tiny wakiwa wameshikana mikono huku wakifuatilia kwa makini utoaji wa Tuzo za BET

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s