ARGENTINA, UBELGIJI ZATINGA ROBO FAINALI, USWISI NA MAREKANI NJE KOMBE LA DUNIA

Straika wa Barcelona na Timu ya Taifa ya Argentina, Lionel Messi akimpongeza Di Maria

Straika wa Barcelona na Timu ya Taifa ya Argentina, Lionel Messi akimpongeza Di Maria

Timu ya Taifa ya Argentina imejikatia tiketi ya moja kwa moja ya kucheza Robo Fainali ya kombe la Dunia baada ya kuibana Uswisi kwa bao moja kwa sifuri.  Timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana dakika 90 za kwanza  kabla ya mchezaji Angel Di Maria kufunga bao pekee na la ushindi ikiwa zimesalia dakika mbili za muda huo wa ziada kukamilika.

Bao hilo lilikuwa ni bao la 151 katika michuano ya mwaka huu ikilinganishwa na mabao 145 yaliyofungwa katika kinyang’anyiro cha miaka iliyopita huko Afrika Kusini japokuwa nyota wa Barcelona, Lionel Messi alikuwa akipewa nafasi ya kung’aa katika mchezo huo  huku akiweka historia ya kufunga kila mechi za Taifa lake,  alionekana kubanwa mbavu na mabeki wa Uswisi.

Wachezaji wa Uswisi, Gokhan Inler na Valon Behrami wakitoka dimbani kwa majonzi baada ya mchezo kuisha

Wachezaji wa Uswisi, Gokhan Inler na Valon Behrami wakitoka dimbani kwa majonzi baada ya kipenga cha mwisho kupulizwa

Mchezo mwingine mabao ya Kevin De Bruyne na Romelu Lukaku yameiwezesha Ubelgiji kutinga hatua ya robo fainali kwa kuilaza Marekani kwa bao mawili kwa moja ikiwa ni mara ya kwanza kwa ubelgiji kufuzu katika hatua hiyo ya robo fainali baada ya kipindi cha miaka 28 .

Huku kipa wa Marekani, Tim Howard akiatajwa kuwa mchezaji bora katika mechi hiyo kufuatia mchezo mzuri aliouonyesha kwa kuokoa mikwaju 16 katika lango lake.

Kevin De Bruyne wa Ubelgiji akipiga shuti kali kuelekea golini mwa Marekani

Kevin De Bruyne wa Ubelgiji akipiga shuti kali kuelekea langoni mwa Marekani

Kipa wa Marekani, Tim Howard akiokoa shuti kali lililopigwa kuelekezwa golini kwake
Kipa wa Marekani, Tim Howard akiokoa shuti kali lililopigwa kuelekezwa golini kwake

De Bruyne

Kevin De Bruyne akishangilia baada ya kuifungia Timu yake bao la ushindi dhidi ya Marekani

Nyanda wa Marekani, Tim Howard akitoka uwanja kwa majonzi baada ya mchezo kumalizika

Nyanda wa Marekani, Tim Howard akitoka uwanjani kwa majonzi baada ya timu yake kushindwa kufuzu

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s