TIMU ZA AFRIKA NJE KOMBE LA DUNIA, ALGERIA NA NIGERIA ZATOLEWA

OzilHatimaye timu zote tano toka barani Afrika zimeaga mashindano ya kombe la Dunia baada ya hapo jana Timu mbili zilizosalia yaani Nigeria na Algeria kufangashiwa virago na Ufaransa pamoja na Ujerumani.

Nigeria ilijikuta ikipoteza mchezo wake huo muhimu wa kufuzu hatua ya robo fainali kwa kukubali kipigo cha bao 2 – 0 dhidi ya Ufaransa huku magoli  yakifungwa na Paul Pogba na lingine la kujifunga toka kwa beki wa Super Eagle ‘Joseph Yobo’ mnamo dakika ya 90′.

Wakati  Algeria ikichezea kichapo  cha bao 2 – 1  toka kwa Ujerumani licha  ya  upinzani mkali waliouonyesha lakini haukuweza kufua dafu na kujikuta wakimaliza dakika 120 kwa kuwapa tiketi wajerumani ya kucheza robo fainali.

Bao la ushindi la Ujerumani  liliwekwa wavuni na Mesut Oezil  huku bao pekee la Algeria likifungwa na Abdelmoumene Djabou.

 

Straika wa Ujerumani, Andre Schuerrle akishangilia baada ya kufunga bao la kuongozea

Straika wa Ujerumani, Andre Schuerrle akishangilia baada ya kufunga bao la kuongozea

Kiungo wa Algeria, Mehdi Mostefa akiwa ameina kwa majonzi baada ya kipenga cha mwisho kupulizwa
Kiungo wa Algeria, Mehdi Mostefa akiwa ameinama kwa majonzi baada ya kipenga cha mwisho kupulizwa

Mesut Ozil akiweka wavuni bao lilliloipa  ushindi timu yake

Mesut Ozil akiweka wavuni bao lililoipa ushindi timu yake

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s