UHOLANZI WAITOA MEXICO KIMAGUMASHI, COSTA RICA YAIFUNGASHA VIRAGO UGIRIKI

Wesley

Wesley Sneijder akishangilia mara baada ya kusawazisha

Kikosi cha Timu ya Taifa ya Uholanzi(Holland) kimeponea chupuchupu kutoka katika hatua ya kumi na sita bora baada ya kuibuka na ushindi dakika za majeruhi wa bao (2 – 1)   dhidi  ya  Mexico  katika  mtanange  uliochezwa  kwenye dimba la Estadio Castelao nchini Brazil.

Kiungo mkabaji wa Colombia, Giovani dos Santos aliweza kuipatia timu yake bao la kuongoza kabla ya kiungo wa kutumainiwa wa Galatasaray,  Wesley Sneijder kusawazisha mnamo dakika ya 88 akifuatiwa na mveterani ‘Klaas Jan Huntelaar‘ aliyefunga bao la pili kwa mkwaju mkali wa penalti baada ya Arjen Robben kudondoshwa na Rafa Marquez wa Mexico ndani ya kumi na nane.

Hata hivyo penalti hiyo ilizua utata huku kocha mkuu wa Mexico ‘Miguel Herrera’ akimtupia lawama refa mreno aliyecheza mchezo huo ‘Pedro Proenca’ kwa kuipendelea Uholanzi kauli iliyoonekana kuuungwa mkono na Robben aliyekiri kuwa haikuwa penalti halali.

Mchezo mwingine uliochezwa hapo jana, ulikuwa  kati ya Costa Rica iliyowafungashia virago mabaharia wa Ugiriki  kwa ushindi wa Penalti 5 dhidi 3 ilizopata  baada ya 120 za mwanzo kutoweza kuzaa matunda na kujikuta wakitoka kutoka suluhu ya goli 1 – 1  huku goli pekee la Costa Rica likifungwa na Brayan Ruiz wakati la Ugiriki likiwekwa kimyani na Sokratis Papastathopoulos.

 

 

Straika wa Uholanzi, Arjen Robben akijiangusha eneo la penalti

Straika wa Uholanzi, Arjen Robben akijiangusha  langoni mwa Mexico

Klaas Jan Huntelaar akishangilia kwa staili ya aina yake baada ya kufunga kwa penalti
Klaas Jan Huntelaar akishangilia kwa staili ya aina yake baada ya kufunga kwa penalti

Hunt Holland

 

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s