URENO YAITUNGUA 2 – 1 GHANA, LAKINI WOTE WAAGA MASHINDANO YA KOMBE LA DUNIA

Asamoah GyanUshindi wa goli 2 – 1 uliopata Ureno dhidi ya Ghana usiku wa kuamkia leo haujaweza kuwasaidia kusonga mbele katika hatua ya 16 bora na kujikuta wakiaga mashindano hayo baada ya kutanguliwa kwa  idadi ya magoli na timu ya Taifa ya Marekani iliyochezea kipigo cha goli 1 toka kwa Ujerumani hapo jana.

CRonaldoStraika wa Ureno(Portugal), Cristiano Ronaldo akiweka mpira wavuni kwenye lango la Ghana

Mshambuliaji wa Ureno na Real Madrid, Cristiano Ronaldo aliweza kuweka rekodi baada ya kuifungia timu yake kwa mara ya kwanza tangu alipoanza kucheza katika timu ya taifa wakati kapten wa Black Stars,  Assamoah Gyan akivunjilia mbali rekodi iliyowekwa na msakata kabumbu wa zamani ‘Roger Mila’  ya kuwa mchezaji wa kwanza wa Afrika  kufunga magoli 5 katika awamu tatu za michuano  ya kombe la Dunia licha ya timu yake kushindwa kusonga mbele.

thomas MullerStraika wa Ujerumani, Thomas Muller akipiga mkwaju mkali ulioweza kuzifumania nyavu za Wamarekani .

Rais wa Marekani, Barack Obama nae pia aliweza kutazama mchezo kati ya Marekani(USA) na Ujerumani akiwa kwenye usafiri wake wa anga anaotumia aina ya Air Force one wakati akitokea Maryland kuelekea Minnesota sambamba na kuwapongeza kwa kuweza kutinga katika hatua ya 16 bora licha ya kipigo cha bao moja walichopokea toka kwa mjerumani Thomas Muller.

Barack Obama akitazama mchezo kati ya marekani na Ujerumani

Barack Obama akitazama mchezo kati ya marekani na Ujerumani ndani ya Air Force One

 

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s