STRAIKA LUIS SUAREZ KUKABILIWA NA KIFUNGO CHA MIAKA 2 ENDAPO ATAPATIKANA NA HATIA YA KUMNG’ATA GIORGIO CHIELLINI WA ITALIA

Suareza akimng'ata

Suareza akimng’ata Giorgio Chiellini

Uruguay imefanikiwa kusonga mbele baada ya kuinyuka Italia kwa goli moja kwa nunge kwenye mechi ambayo mshambuliaji hatari wa Uruguay na Liverpool, Luis Suarez alikutana na shutma nyingine ya kumng’ata mchezaji Giorgio Chiellini.

Straika huyo mtukutu anakabiliwa na adhabu kali ya kutoshuka dimbani kwa muda mrefu ikiwa ni pamoja na kukosa mechio zilizosalia za michuano ya kombe la Dunia endapo atapatikana na hatia ya kumuuma meno mchezaji huyo wa Italia.

Shirikisho la kandanda FIFA limeanzisha harakati za kumuadhibu mchezaji huyo aliyemng’ata meno mchezaji mwenzie hapo jana ambapo Uruguay ikichomoza na ushindi wa bao 1 kwa bila hata hivyo Gelini amedai kuwa Suarez alimng’ata begani licha ya mruguay huyo kudai kuwa yeye ndiye aliyefanyiwa madhambi.

Chiellini akiugulia maumivu baada ya kuumwa meno na Straika huyo wa timu ya Taifa ya Uruguay na Liverpool

Chiellini akiugulia maumivu baada ya kuumwa meno na Straika huyo wa timu ya Taifa ya Uruguay na Liverpool

Suarez mwenye umri wa miaka 27 huenda akasimamishwa kutoshuka dimbani katika mechi 24 au kuwa nje ya dimba kwa kipindi cha miaka miwili.

Mwamuzi aliyesimamia mecho hiyo kutoka Mexico, Marc Rodriguez hakuchukua hatua yoyote kufuatia kutoona kitendo hicho lakini FIFA bado inamamlaka ya kumuadhibu Suarez huku   klabu yake ya Liverpool imesema itakaa na kujadili mustakabali wa mchezaji huyo.

Hii sio mara ya kwanza kwa Suarez kufanya kosa kama  hilo, kwani hata mwaka jana aliwahi kumuuma meno mchezaji Branislav Ivanovic wakati Liverpool ilipoumana na Chelsea.

Suarez Uruguay

Straika Mtukutu, Luis Suarez akiugulia baada ya kumng’ata Chiellini

Wakati vioja hivyo vikiendelea, timu ya Taifa ya England imejikuta ikiaga mashindano hayo baada ya kubanwa mbavu na Costa Rica kwa suluhu isiyokuwa na goli.

Huku wawakilishi wa Afrika, timu ya Ivory Coast waliokuwa wanahitaji suluhu, kupoteza nafasi hiyo baada ya kufungwa goli dakika za majeruhi kwa mkwaju wa penalti na kujikuta wachezea kichapo cha mbili kwa moja na kuaga mashindano haya wakati Japan nao wakilambishwa mabao 4 – 1 dhidi ya vinara Colombia.

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s