STRAIKA WA URENO(PORTUGAL), CRISTIANO RONALDO ANYOA KIDUKU MASAA MACHACHE KABLA YA TIMU YAKE KUIKABILI GHANA

 

Cristiano Ronaldo ndani ya kiduku

Straika wa ureno, Cristiano Ronaldo akiwa mazoezini ndani ya staili mpya ya nywele ‘kiduku’

Huenda ukashangazwa na staili  mpya ya nywele maarufu kama Kiduku aliyonyoa Straika wa Timu ya Taifa ya Ureno(Portugal) na Real Madrid, Cristiano Ronaldo wakati timu yake itakaposhuka dimbani usiku wa leo kuvaana na kikosi hatari cha Black Stars(Ghana)  katika mtanange utakaochezwa kwenye uwanja wa Estadio Nacional De Brasilia.

Hata hivyo bado haijaweza kufahamika mreno huyo ameamua kufanya hivyo kwa lengo gani huku mamilioni ya mashabiki toka barani Afrika  na Dunia kote wakisubiria kwa hamu mchezo huo wa kundi ‘G’ unaotarajiwa kuanza majira ya saa 1 jioni kwa saa za Afrika Mashariki  ambapo Ghana inahitaji ushindi mnono ili iweze kufuzu katika hatua ya 16 bora.

Cristiano Ureno

Hapa akifanya mazoezi na wachezaji wenzake wa timu ya Taifa ya Ureno(Portugal)

CRonaldo Ronaldo Kiduku

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s