MWANAMKE WA SUDAN ALIYEASI DINI AKAMATWA TENA

Meriam Sudan

Meriam aliyemshika mtoto akiwa na mumewe Daniel Wani(Wa Kwanza Kushoto) pamoja na ndugu, jamaa na marafiki

Mara baada ya mahakama ya rufaa (kumuachia huru) kwa kutoa uamuzi mpya unaopinga hukumu aliyopewa mwanamama Meriam Yahya Ibrahim, aliyehukumiwa kifo kwa kunyongwa nchini Sudan kwa tuhuma za kubadili dini, mwanamama huyo amekamatwa tena na polisi wa nchini humo akiwa uwanja wa ndege kuelekea Marekani pamoja na mumewe, Daniel Mani, ambapo aliamini angepata pumziko kutokana na misukosuko aliyopata.

Mumewe, ambaye ni raia wa Marekani ameelezea kuwa kulikuwa na mvutano kwenye uwanja wa ndege wa Khartoum, ambapo alikuwa ameongozana na mkewe pamoja na watoto wao wawili kuelekea Marekani, kabla maafisa usalama zaidi ya 40 kujitokeza na kumkamata upya Meriam kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kughushi nyaraka za safari.

Hukumu ya Meriam ambayo imezua mijadala ya kimataifa, ilipelekea mashinikizo kadhaa kutoka jumuiya mbalimbali, ikiwemo baraza la Congress nchini Marekani, ambapo wajumbe 38 walisaini waraka wakitaka taifa lao lichukue hatua kuhakikisha usalama wa Meriam na watoto wake wawili, ambapo hivi karibuni alijifungua mtoto wa pili, Maya, akiwa gerezani – huku ikiripotiwa kuwa akiwa kwenye uchungu, bado miguu yake ilikuwa imefungwa minyororo.

Meriam, mwenye umri wa miaka 27 – alikamatwa kwa mara ya kwanza Agosti 2013, baada ya ndugu wa baba yake kuripoti kwamba amezini (baada ya kuolewa na Wani, ambaye ni mkristo), ambapo katika utetezi wake, Meriama ameeleza bayana kwamba yeye ni mkristo, kama ambavyo mama yake amemkuza, baada ya baba yake, ambaye ni muislamu, kuiacha familia hiyo tokea Meriam  akiwa mdogo.

Miongoni mwa viongozi wa mataifa makubwa walioolani ni pamoja na waziri wa mambo ya nje wa Australia, Bi Julie Bishop, waziri mkuu wa zamani wa Uingereza, Tony Blair pamoja na waziri mkuu wa sasa, David Cameron. Kiongozi mwingine ni katibu wa taifa la Marekani, Bi Hillary Clinton.

Kwa sasa ripoti zaidi zinasubiriwa, ambapo dunia nzima inalitazama hili suala, ambapo ni chini ya masaa 24 tokea taarifa za kuachiwa zitolewe na mwanasheria wa Meriam, Mohaned Mustafa El-Nour. Taarifa zaidi zinaeleza kuwa Meriam amekamatwa upya ili kutazama usahihi wa hati zake za kusafiria na kwamba walishikiliwa kwa masaa 24.

-bbc.co.uk

Advertisements

One thought on “MWANAMKE WA SUDAN ALIYEASI DINI AKAMATWA TENA

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s