BRAZIL YAIFUNGISHA VIRAGO CAMEROON KWA KIPIGO CHA GOLI 4 – 1, UHOLANZI YAILAZA 2 – 0 CHILE

 

Straika wa Brazil Neymar Jr akishangilia baada ya kutupia wavuni goli la kwanza

Straika wa Brazil Neymar Jr akishangilia baada ya kutupia wavuni goli la kwanza

Wenyeji Brazil jana wamekamilisha mechi zao za kundi A, kwa ushindi mujarabu wa mabao 4 – 1 dhidi ya Cameroon kwenye uwanja wa Estadio Nacional de Brasilia, mshambuliaji tegemea kabisa Neymar Jr au shujaa wa Brazil alifunga mabao mawili kunako dakika ya 17 na 34 wakati mabao mengine yakifungwa na Fred  katika dakika ya 49 na Fernandinho kunako dakika ya 84 huku bao pekee la Simba wasiofungika likiwekwa kimyani na Joel Matip na kuifanya Cameroon kuwa timu ya kwanza toka Afrika kuaga michuano hiyo ya kombe la Dunia.

Matip Cameroon

Joel Matip wa Cameroon(Katikati) akishangilia baada ya kusawazisha goli dhidi ya Brazil

Taarifa nyingine ni kwamba kikosi cha timu ya taifa ya Uholanzi imefanikiwa kutinga hatua ya 16 bora hapo jana baada ya kushinda mechi zake zote za kundi B ikimaliza na ushindi wa mabao 2 – 0 dhidi ya Chile huku magoli hayo yakifungwa na Leroy Fer pamoja  na Memphis Depay.

Wachezaji wa Timu ya taifa ya Uholand(Holland) wwakishangilia baada ya kuigalagaza Bao 2 - 0 Chile na hivyo kufanikiwa kutinga hatua ya 16 bora

Wachezaji wa Timu ya taifa ya Uholand(Holland) wwakishangilia baada ya kuigalagaza Bao 2 – 0 Chile na hivyo kufanikiwa kutinga hatua ya 16 bora

Hata hivyo licha ya ushindi huo mnono, kocha mkuu wa wadachi hao, Luis Van Gaal amelilalamikia shirikisho la mpira Duniani  FIFA akisema kwamba ratiba ya kombe hili la Dunia imepangwa kwa hila na kuongezea kuwa imekuwa ikiwapendelea sana Brazil.

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s