BOW WOW ABADILI JINA LAKE LA KISANII, KUANZA KUITWA ‘SHAD MOSS’

Shad MossMkali wa muziki wa kufokafoka toka Mamtoni, Bow Wow ameamua kufanya mabadiliko makubwa ya jina lililomtambulisha katika medani ya muziki wa kimataifa kipindi hicho akijulikana kama Lil Bow Wow kabla ya kubadili na kuitwa Bow wow na sasa ametangaza rasmi ujio wa jina jipya atakalokuwa akitumia kunako kwa steji na maeneo mengine ya kumuingizia mkate wake wa kila siku.

Habari zilizotapakaa kwenye mitandao mingi wikiendi iliyopita zinaeleza kuwa rapa huyo amewambia mashabiki zake kuwa baada ya tuzo za BET zitakazofanyika Jumapili ya Juni 29 mwaka huu,  jina lake la kisanii litakuwa ‘Shad Moss’ jina alilopewa na wazazi wake.

”’Tangazo : Baada ya Tuzo za BET sitakuwa nikitumia tena jina la Bow Wow! nitatumia  jina langu la halisi ”Shad Moss” tumeweka historia kubwa kama bow wow. Sasa ni muda wa kufungua ukurasa mpya na changamoto. Bow wow haliendani na jinsi nilivyo kwa sasa. Mimi ni baba, mfanyabiashara, mtangazaji, muigizaji na Rapa! Muda wa MR Moss kuchukua hatamu yake” alisema Bow Wow kwenye video fupi aliyoipakia(upload) kwenye ukurasa wake wa instagram.

 

 

 

 

 

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s