GHANA YATOKA SARE YA 2 – 2 NA GERMANY, MESSI AIBEBA ARGENTINA, WAITANDIKA 1 – 0 IRAN

Messi

Mshambuliaji hatari wa klabu ya Barcelona na Timu ya Taifa ya Argentina, Lionel Messi akishangilia kwa furaha bao alilofunga dakika za majeruhi na wachezaji wenzake

Iran imejiweka katika mazingira mgumu ya kusonga  mbele,  baada ya kukubali  kipigo cha bao 1 – 0 dhidi ya  Argentina katika mchezo wa kundi ”F” uliochezwa kwenye uwanja wa Estadio Mineirao.  Licha ya kuonyesha upinzani mkali haikuweza kuwa mwarobaini kwa  Argentina huku bao pekee likifungwa na mpachika magoli wa Barcelona, Lionel Messi mnamo dakika za majeruhi.

Goli Kipa wa Iran, Alireza Haghighi akiusindikiza kwa macho mpira ukielekea wavuni baada ya kupigwa kiufundi na Messi mnamo dakika ya 90'

Goli Kipa wa Iran, Alireza Haghighi akiusindikiza kwa macho mpira ukielekea wavuni baada ya kupigwa kiufundi na Messi mnamo dakika ya 90′

Matokeo ya mchezo huo yameipa tiketi  Argentina ya kusonga mbele katika hatua ya 16 bora huku ikiwa tayari imeshashinda michezo miwili na kubakisha mmoja wakati Super Eagle wa Nigeria wakiwa na kibarua kigumu usiku huu  cha kuisambaratisha ngome ya Bosnia and Herzegovina ili kuweza kujiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu katika hatua ya makundi.

Messi Ar

Straika wa Timu ya Taifa ya Argentina, Lionel Messi akilia kwa furaha baada ya kipenga cha mwisho kupulizwa na hivyo kuipatia timu yake pointi 3 muhimu

Mchezo mwingine uliochezwa ulikuwa ni kati ya Germany na Ghana ambapo mpaka kipenga cha mwisho kinapulizwa matokeo yalimalizika kwa suluhu ya mabao mawili kwa mawili huku Ujerumani wakiwa ndio wa kwanza kuzifumania nyavu za Black Stars kupitia Mario Goetze kabla ya kusawazishwa na Andre Ayew mnamo dk ya 54′ na kisha Asamoah Gyan kuongeza bao lingine dakika ya 63′ lakini haikuwa bahati kwa wawakilishi hao wa Afrika baada ya Miroslav Klose kusawazisha na kufanya matokeo kuwa droo.

Mario Goetze nakishangilia baada ya kuitundikia timu yake ya Germany bao la kwanza

Mario Goetze wa Ujerumani akishangilia baada ya kutundikia  bao la kwanza

Andre Ayew wa Ghana akishangilia baada ya kuisawazishia timu yake goli la kwanza

Mchezaji wa Ghana, Andre Ayew baada ya kuisawazishia timu yake goli la kwanza

 

 Asamoah Gyan akishangilia sambamba na wachezaji wenzake wa Ghana baada kuipachikia timu yake bao la pili

Asamoah Gyan akicheza sambamba na wachezaji wenzake wa Ghana baada kuipachikia timu yake bao la pili

Kipa wa Timu ya Taifa ya Ghana 'Fatau Dauda' akiuangalia kwa uchungu mpira uliopigwa na  Klose ukiingia goli

Kipa wa Timu ya Taifa ya Ghana ‘Fatau Dauda’ akiuangalia kwa uchungu mpira uliopigwa na Klose ukiingia golini kwake na kugeuza matokeo

 

Straika wa ujerumani, Miloslav Klose akiruka beki baada ya kusawazisha bao la pili

Straika wa ujerumani, Miloslav Klose akiruka beki baada ya kusawazisha bao la pili na matokeo kumalizika kwa suluhu ya 2 – 2

 

Mchezaji wa Ghana 'Jerome  Boateng'(kushoto) akisalimia na kaka yake Kevin - Prince Boateng Jr(kulia) wa timu ya Taifa ya Ghana

Mchezaji wa Ghana ‘Jerome Boateng'(kushoto) akisalimia na kaka yake Kevin – Prince Boateng Jr(kulia) wa timu ya Taifa ya Ghana baada ya mchezo kumalizika

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s