KIM KARDASHIAN ATANGAZA UJIO WA GEMU YAKE MPYA ITAKAYOANZA KUPATIKANA KWENYE SIMU ZA MKONONI

Kim K

Mke wa ndoa wa Rapa Kanye west, mwanamitindo daraja la kwanza Kim Kardashian ameendelea kutunisha akaunti zake za benki baada ya kujikita kwenye biashara ya gemu itakayokuwa ikipatikana kwenye simu za mkononi zenye Google Play na App Store kupitia applikesheni mpya ya Hoolywood.

Gemu hiyo inatarajiwa kuzinduliwa wiki ijayo, ambapo  mchezaji ataweza  kuvaa uhusika wa maisha ya Kimmie ikiwemo kuanzisha mahusiano, kununua bidhaa kama vile nguo, vipodozi, viatu, vinywaji, kwenda sehemu za kula bata pamoja na vikolombwezo vingine kibao.

”Nina furaha kuitambulisha gemu mpya #KimKardashianGame itakayozinduliwa wiki ijayo kwenye App Store na Google Play! Tazama kionjo chake” aliandika Kim K….

Hii huenda ikawa habari nzuri kwa mashabiki na wapenzi wa Kim wanaotumia  simu aina ya iPhone au Samsung zenye Google Play na App Store.

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s