HAT-TRICK YA MULLER WA UJERUMANI YAILOWESHA URENO, GHANA YATANDIKWA 2 -1 NA MAREKANI, NIGERIA NA IRAN ZATOKA SARE TASA

Thomas Muller akishangilia baada ya kupachika bao la kwanza

Ushindi wa mabao  4 – 0 iliyoupata timu ya taifa ya Ujerumani dhidi ya Ureno(portugal) kwenye dimba la Arena Fonte Nova umeiwezesha kunyakua pointi tatu muhimu na kukaa kileleni mwa kundi ‘G’ sambamba na Marekani(USA) kwa tofauti ya magoli mawili.

Straika wa Bayern Munich, Thomas Muller aliweza kuandika rekodi mpya  ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao matatu  tangu kuanza kwa michuano hiyo huku bao lingine likifungwa na Mats Hummels na hatimaye mchezo kumalizika kwa Ujerumani kuibuka na ushindi wa goli 4 wakati Ureno wakiambulia patupu licha ya uwepo wa mshambuliaji wao tegemezi Cristiano Ronaldo.

Seeing red: Pepe butts Muller while the German is sat on the floor and is sent off

Beki wa kati wa klabu ya Madrid na timu ya taifa Ureno Pepe akimzonga straika wa Ujerumani, Thomas Muller baada ya kumchezea vibaya na kujikuta akiambulia kadi nyekundu

Ghana

Wachezaji wa Ghana wakiokoa mpira kwenye ngome yao iliyokuwa ikishambuliwa na kikosi cha Marekani

Mchezo mwingine uliokuwa wa vuta nikuvute ni ule uliowakutanisha timu ya taifa ya Nigeria ”The Super Eagle” waliotoka sare tasa ya bila kufungana na Iran katika mtanange uliochezwa kwenye uwanja wa Arena da Baixada (Joaquim Americo) huku wawakilishi hao kutoka Afrika wakijikuta wakishindwa kutumia vyema nafasi nyingi walizopata.

Wawakilishi wengine wa Afrika, timu ya taifa ya Ghana ilijikuta ikichezea kichapo cha bao 2 – 1 kutoka kwa timu ya taifa ya Marekani(USA) kupitia wachezaji wake Clint Dempsey pamoja na John Brooks huku goli pekee la Ghana likifungwa na Andre Ayew. Tazama Video za Magoli Hapo Chini

 

 

 

Advertisements

One thought on “HAT-TRICK YA MULLER WA UJERUMANI YAILOWESHA URENO, GHANA YATANDIKWA 2 -1 NA MAREKANI, NIGERIA NA IRAN ZATOKA SARE TASA

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s