2014 FIFA WORLD CUP : BRAZIL YAANZA VIZURI, YAIBAMIZA BAO 3 -1 CROATIA

Marcelo

Mchezaji wa Brazil, Marcelo akiutazama mpira aliojifunga wakati akijaribu kuikoa

Wanasema mcheza kwao hutuzwa, Kikosi cha timu ya Taifa ya Brazil ambao ndio wenyeji na waandaaji wa michuano ya kombe la Dunia kwa mwaka 2014, wameweza kuibuka kidedea baada ya kuikandamiza bao 3 – 1 timu ya Taifa ya Croatia katika mchezo wa kwanza wa ufunguzi wa michuano hiyo wa kundi ”A” uliochezwa hapo jana kwenye dimba la Arena Corithians mjini Sao Paulo nchini humo.

Katika mchezo huo Croatia ndio waliotangulia kuzifuma nyavu za wakali hao wa samba kwa goli la kujifunga kutoka kwa  Marcelo Junior mnamo dakika ya 11 kipindi cha kwanza cha mchezo kabla ya Neymar kusawazisha dakika ya 29 na kufanya matokeo kwenda sare ya 1 – 1 mpaka mapumziko.

Neymar BrazilStraika wa Brazil, Neymar akitupia wavuni mpira wa adhabu

 

Angwe ya pili iliyokuwa ya vuta nikuvute, iliweza kuzaa matunda kwa Brazil kufuatia mpira wa adhabu uliopigwa na Neymar dk ya 71, kabla ya kiungo mkabaji wa Chelsea Oscar dos Santos Emboaba Júnior kukamilisha idadi hiyo ya magoli baada ya kutundika wavuni bao la 3 katika dakika za majeruhi na hatimaye mchezo kumalizika kwa Brazil kujinyakulia Pointi 3 muhimu dhidi ya wapinzani wao Croatia.

OscarNi Upendo Tuu, Oscar akishangilia baada ya kuweka wavuni bao 3 mnamo dakika ya 90

Kwa sasa Brazil inaongoza kundi A ikiwa kileleni kwa pointi 3,  huku macho ya waafrika yakitegemea kuona makubwa zaidi kutoka kwa  Timu ya Taifa ya Cameroon(The Indomitable Lions) watakaoshuka dimbani hii leo kumenyana na Mexico.

Cameroon

Tazama Video za magoli hapo chini

 


Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s